Mamlaka ya Mapato Tanzania imewarahisishia wamiliki wa magari au Wanaoingiza Magari kutoka Nje ya nchi kwa kuanzisha mfumo wa kucalcute makadirio ya Ushuru wa gari kwa kutumia mfumo wa Used Motor Vehicle Valuation System. Mfumo huu unawarahisishia wamiliki wa gari kukadiria kiwango cha kodi kwa gari zilizotumika.
Calculator ya Ushuru wa Magari TRA ninini?
Calculator ya Ushuru wa Magari ya TRA ni zana ya mtandao inayowawezesha wamiliki wa magari, wataalamu wa forodha, na biashara zinazohusiana na usafiri, kujua kwa urahisi kiasi cha ushuru wa gari kinachopaswa kulipwa.
Kiasi cha ushuru wa gari kinategemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:
Aina ya gari: Kama gari ni la abiria au la mizigo.
Ujazo wa injini: Gari lenye injini kubwa linaweza kuwa na ushuru mkubwa zaidi.
Umri wa gari: Magari mapya mara nyingi hulipiwa ushuru tofauti na magari ya zamani.
Thamani ya gari: Hii inaathiri kodi ya forodha na ushuru mwingine wa kibiashara.
Misingi ya kodi nyingine: Zana hii inachukua pia vigezo vya kodi za ziada kama vile VAT na Excise Duty.
Jinsi ya Kutumia Kikokotoo cha Ushuru wa Magari
Kikokotoo cha ushuru wa magari cha TRA kinapatikana kwenye tovuti yao rasmi. Ili kutumia kikokotoo hiki, fuata hatua zifuatazo:
- Chagua Maelezo ya Gari:
- Aina ya Gari: Chagua aina ya gari kutoka kwenye orodha (mfano, TOYOTA, NISSAN, BMW).
- Modeli na Mwili: Chagua modeli na aina ya mwili wa gari.
- Mwaka wa Utengenezaji: Chagua mwaka ambao gari lilitengenezwa.
- Nchi ya Asili: Chagua nchi ambako gari lilitengenezwa.
- Aina ya Mafuta: Chagua aina ya mafuta yanayotumika kwenye gari (mfano, petroli, dizeli).
- Uwezo wa Injini: Chagua uwezo wa injini ya gari (mfano, 1500cc, 2000cc).
- Pata Thamani ya Gari:
- Baada ya kujaza maelezo yote ya gari, bonyeza kitufe cha “Pata Thamani” ili kupata thamani ya gari lako.
- Hesabu Ushuru:
- Mfumo utakuonyesha thamani ya gari na kiasi cha ushuru kinachopaswa kulipwa.
Mfano wa Ukokotoaji wa Ushuru
Ili kuelewa vizuri jinsi ya kukokotoa ushuru wa gari, tutaangalia mifano miwili ya magari tofauti.
Mfano 1: Toyota Corolla 2015
Kipengele | Maelezo |
---|---|
Aina ya Gari | Toyota |
Modeli na Mwili | Corolla |
Mwaka wa Utengenezaji | 2015 |
Nchi ya Asili | Japan |
Aina ya Mafuta | Petroli |
Uwezo wa Injini | 1500cc |
Baada ya kujaza maelezo haya kwenye kikokotoo, thamani ya gari inaweza kuwa TZS 20,000,000. Ushuru wa kuingiza gari hili unaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Ushuru wa Forodha: 25% ya thamani ya gari = TZS 5,000,000
- Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT): 18% ya (Thamani ya Gari + Ushuru wa Forodha) = 18% ya TZS 25,000,000 = TZS 4,500,000
- Kodi ya Mapato: 10% ya (Thamani ya Gari + Ushuru wa Forodha + VAT) = 10% ya TZS 29,500,000 = TZS 2,950,000
Mfano 2: Nissan X-Trail 2018
Kipengele | Maelezo |
---|---|
Aina ya Gari | Nissan |
Modeli na Mwili | X-Trail |
Mwaka wa Utengenezaji | 2018 |
Nchi ya Asili | Japan |
Aina ya Mafuta | Dizeli |
Uwezo wa Injini | 2000cc |
Baada ya kujaza maelezo haya kwenye kikokotoo, thamani ya gari inaweza kuwa TZS 35,000,000. Ushuru wa kuingiza gari hili unaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Ushuru wa Forodha: 25% ya thamani ya gari = TZS 8,750,000
- Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT): 18% ya (Thamani ya Gari + Ushuru wa Forodha) = 18% ya TZS 43,750,000 = TZS 7,875,000
- Kodi ya Mapato: 10% ya (Thamani ya Gari + Ushuru wa Forodha + VAT) = 10% ya TZS 51,625,000 = TZS 5,162,500
Faida za Kutumia Calculator ya Ushuru wa Magari
Kuna faida nyingi za kutumia Calculator ya Ushuru wa Magari ya TRA. Hizi ni baadhi ya manufaa kuu:
a) Usahihi wa Matokeo
Calculator hii inatoa matokeo sahihi kulingana na taarifa za gari lako, hivyo unapolipa ushuru unakuwa na uhakika kuwa unalipa kiasi cha kodi kilichohesabiwa kwa usahihi.
b) Kuepuka Faini
Kwa kutumia calculator, utajua ni kiasi gani cha ushuru kinachohitajika na tarehe ya mwisho ya kulipa. Hii inasaidia kuepuka faini au adhabu zinazoweza kutolewa kwa kushindwa kulipa kwa wakati.
c) Kuokoa Muda
Calculator ya TRA ni ya haraka na rahisi kutumia, hivyo hutoa nafasi kwa wamiliki wa magari kutimiza majukumu yao kwa haraka bila ya kutumia muda mwingi kwenye foleni au ofisi za TRA.
d) Huduma ya Kidijitali
Calculator hii ni sehemu ya juhudi za TRA kuboresha huduma za serikali kwa kutumia teknolojia. Wamiliki wa magari wanapata huduma ya haraka na rahisi bila ya kufika ofisini, hivyo inarahisisha mchakato wa malipo.
e) Kupata Habari Kamili
Unapata taarifa zote za kodi zinazohusiana na gari lako, kama vile VAT, import duty, na excise duty. Hii ni muhimu kwa biashara za kuingiza magari, kwani zinaweza kujua kwa urahisi kiasi cha kodi wanachotakiwa kulipa.
Soma Hii :jinsi ya kuangalia ushuru wa gari yanayoingizwa nchini
Mambo ya Kuangalia Kabla ya Kutumia Calculator ya Ushuru wa Magari
Kabla ya kutumia Calculator ya Ushuru wa Magari, hakikisha yafuatayo:
Thamani ya Gari: Hakikisha kuwa thamani ya gari lako inaakisi bei halisi sokoni ili usije kulipia kodi nyingi.
Aina ya Gari: Elewa ni aina gani ya gari unalolipia ushuru (lori, gari la abiria, au gari la biashara).
Injini: Ujazo wa injini unaathiri kiasi cha ushuru, hivyo hakikisha kuwa umekadiria kwa usahihi.