Mifumo ya Maisha inabadilika kila siku hasa utokana na Ukuaji wa Teknolojia Miaka ya sasa hivi huhitaji kuajiriwa au kujiajiri kwa kufungua ofisi unaweza tengeneza pesa nyingi sana kwa Kufanya Biashara Mtandaoni Hapa tumekuwekea Aina kadhaa ya Biashara unazoweza kuzifanya mtandaoni na kukuingizia pesa nyingi kwa mwezi.
Biashara za mtandaoni zinazoingiza pesa
Katika Orodha ya Hizi Biashara unaweza ukachagua Moja ukaiwekea muda na kuifanya kwa ustadi na ikakutoa kimaisha.
Kuanzisha Tovuti au Blog

Kuanza tovuti au blog ni hatua nzuri kama unataka kushiriki maarifa yako, kuanzisha biashara mtandaoni, au kujenga jamii.Kupitia Blog unaweza kutengeneza pesa kupitia Matangazo ya Google AdSense ,Affiliate Marketing,Kuuza Bidhaa na Huduma Zako kama vile hopify au WooCommerce ,Uandishi wa Kibiashara (Sponsored Posts),Kufundisha Ujuzu mtandaoni,Kuuza Nafasi za Matangazo (Banner Ads)
Kuanzisha YouTube Channel
Kupata pesa kupitia channel ya YouTube ni ndoto ya wengi, na kwa hakika ni njia nzuri ya kupata kipato kutoka kwa kazi yako ya ubunifu. Kupitia Youtube Channel unaweza pata Pesa kupitia njia zifuatazo Matangazo ya YouTube (Adsense),Affiliate Marketing Mashirika maarufu ya affiliate ni Amazon Associates, ClickBank, ShareASale, na CJ Affiliate,Kwa Live Streams ,Memberships na Channel Subscriptions,Kufanya Ushirikiano na Brands (Sponsorships) Soma zaid=> Jinsi ya Kutengeneza Pesa Kupitia Mtandao wa Youtube
Kutafuta Masoko Kwa Niaba ya Makampuni (Affiliate Marketing)
Affiliate Marketing ni mbinu ya kidigitali ya kuuza bidhaa au huduma ambapo mtu (affiliate) anapata kamisheni kwa kila mauzo, uandikishaji, au kitendo fulani (kama vile kujisajili) kinachotokea kupitia kiunga chake cha kipekee (affiliate link).
Jinsi Inavyofanya Kazi:
- Mtu anajiunga na programu ya affiliate – Hii inaweza kuwa kupitia kampuni moja kwa moja au kupitia mitandao ya affiliate kama Amazon Associates, ClickBank, au CJ Affiliate.
- Kupata kiunga cha kipekee – Unapojisajili, unapata linki ya kipekee ya kushiriki na wateja wako.
- Kushiriki linki – Unaweza kuiweka kwenye blogu, mitandao ya kijamii, YouTube, au hata kutuma kwa marafiki.
- Watu wanabonyeza na kununua – Ikiwa mtu atanunua kupitia link yako, unapata asilimia fulani ya mauzo kama kamisheni.
- Kulipwa – Kampuni hulipa affiliates kulingana na mapato yao ndani ya muda uliowekwa (kila wiki, kila mwezi, n.k.).
Ushawishi Kwenye Mitandao ya Kijamii (Social media influencer)
Kwa sasa kama umekuwa ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram lazima unajua kuwa kuna baadhi ya watu wanafanya matangazo ya makampuni fulani kupitia akaunti zao hii ndio inaitwa social media influencer, hapa sisemi matangazo ya vipodozi au matangazo madogo madogo bali mara nyingi watu hawa hupewa bidhaa na makampuni makubwa kuweza kujaribu au kutumia na baadae kutangaza kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii. Lakini biashara hii kama zilivyo biashara nyingine nayo pia inakuja na changamoto.
Ili kuweza kufanya biashara hii unahitaji kuwa na wafuasi wengi na pia unahitaji kuhakikisha wewe mwenyewe unajiweka kwenye mazingira bora ya kushawishi kampuni kuweza kufanya kazi na wewe, akaunti yako isiwe yenye kuvunja sheria za nchi au kukiuka maadili kwa namna moja amba nyingine lakini kikubwa kabisa unatakiwa kuwa na ushawishi mkubwa kupitia mitandao yako hiyo.
Kuwanunulia Wateja Bidhaa Kutoka Mtandaoni (Drop shipping)
Kama wewe ni mpenzi wa biashara mtandaon basi lazima utakuwa kwa namna moja ama nyingine umeshawahi kuwaza kununua kitu kutoka mtandaoni, lakini kutokana na sababu kama njia rahisi za malipo pamoja na njia za kufanya mzigo kukufikia kwa urahisi basi unakuta hatua hii ya kununua kitu inakuwa ni ngumu sana.
Ndio maana biashara ya kununulia watu vitu kutoka mtandaoni ni moja ya biashara bora sana kwa sasa hapa Tanzania. Biashara hii inahusisha kununua bidhaa kwenye tovuti kubwa kama vile Amazon, Ebay na nyingine kama hizo na kusafirisha bidhaa hizo moja kwa moja kwa mteja bila mteja kuwa na mawasiliano na kampuni husika, mteja hukulipa wewe kiasi fulani cha pesa ambacho hichi hutosha kulipia gharama zote pamoja na wewe kupata faida kwa kiasi fulani.
Mara tu mzigo unapofika mteja huja kuchukua kwenye ofisi zako au huletewa na kampuni za usafirishaji ambazo unakuwa unafanya nazo kazi, uzuri wa biashara hii unaweza kufanya bila hata ya kuwa na ofisi lakini unahitaji kuwa na uaminifu mkubwa ambao huu unapatikana kwa kuwa na jina kubwa pamoja na kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu kidogo.
Biashara Nyingine Zinazoweza kukuingizia Pesa Mtandaoni
Kuandika na Kuhariri kwa Kujitegemea
Msaidizi wa Mtandao
Usimamizi wa Media Jamii
Podcasting
Mafunzo ya Mitandao ya Kijamii
Mafunzo ya Lugha Mtandaoni