Kila mfanyabiashara ana ndoto ya kupata kipato kizuri cha kila siku – kiasi ambacho kinaweza kutimiza mahitaji ya msingi, kuweka akiba na hata kuwekeza zaidi. Lakini je, unajua kuwa kuna biashara halali, za kawaida kabisa, ambazo unaweza kuanzisha na kupata faida ya hadi laki moja (100,000 TZS) kwa siku? Ndio! Na si lazima uwe bilionea kuanza nazo.
Aina za Biashara
1. Biashara ya Chakula (Restaurant au Catering Services)
Huduma ya chakula ni moja ya biashara zenye mzunguko wa pesa kila siku. Ukiweza kutoa chakula kitamu, safi, na kwa bei nzuri – wateja hawatakosekana.
Aina ya vyakula vinavyolipa:
Wali, Maharage, Nyama, Ndizi, Pilau
Uji wa asubuhi, vitafunwa
Lunch box kwa ofisi na mashirika
Faida: Sahani moja ya chakula inaweza kukuingizia faida ya TZS 1,000 – 3,000. Ukiuza sahani 50–100, faida ya laki moja ni halisi.
Mtaji wa kuanzia: TZS 500,000 – 2,000,000 (kutegemea ukubwa)
2. Biashara ya Uuzaji wa Mavazi (Nguo na Viatu)
Nguo ni hitaji la kila siku, na watu wapo tayari kulipia mtindo na muonekano mzuri.
Uza nguo za watoto, ofisini, mitumba bora, au nguo za harusi.
Unaweza kuuza moja kwa moja sokoni, mtaani, au kwa njia ya mtandao (Instagram, TikTok).
Faida: Kila nguo inaweza kuwa na faida ya TZS 5,000 – 20,000. Ukiuza vipande 10 tu, unaweza kufika au kuvuka laki moja.
Mtaji wa kuanzia: TZS 800,000 – 3,000,000
3. Saluni Kubwa au Huduma za Urembo na Nywele
Saluni zenye huduma nyingi (kusuka, kupaka rangi, pedicure, massage, dreadlocks n.k.) zina uwezo wa kuingiza mapato makubwa kwa siku moja.
Faida: Huduma moja inaweza kuwa na faida ya TZS 5,000 – 15,000. Ukihudumia wateja 10–15 kwa siku, unaweza kupata faida ya TZS 100,000 au zaidi.
Mtaji wa kuanzia: TZS 1,500,000 – 5,000,000
4. Biashara ya Vipodozi na Perfume Original
Watu wengi hupenda bidhaa za urembo na kujipamba, hasa wanawake.
Uza bidhaa kama perfume original, body spray, lotions, make up kits, na sabuni za ngozi.
Pata bidhaa zako kwa bei ya jumla na uuze kwa rejareja.
Faida: Faida ya bidhaa moja inaweza kuwa TZS 2,000 – 10,000. Ukiuza vipande 15–30, faida ya laki moja inafikiwa.
Mtaji wa kuanzia: TZS 1,000,000 – 4,000,000
Soma Hii : Biashara yenye faida Elfu kumi 10000 kwa Siku
5. Biashara ya Kilimo cha Kisasa cha Mboga Mboga na Maua (Greenhouse)
Greenhouse farming huzaa kwa haraka, kwa ubora na kwa bei nzuri sokoni.
Mimea Inayolipa Sana:
Nyanya, pilipili hoho, lettuce, strawberry
Maua ya kupamba au ya ibada
Faida: Huu ni mradi wenye mzunguko wa faida mkubwa sana, ambapo kwa soko la uhakika, unaweza kuuza mazao ya laki moja kwa siku au zaidi.
Mtaji wa kuanzia: TZS 3,000,000 – 10,000,000 (kutegemea ukubwa wa greenhouse)
6. Uuzaji wa Vifaa vya Simu na Teknolojia (Accessories Shop)
Biashara ya kuuza vifaa vya simu kama earphones, chargers, covers, power banks, USB cables nk.
Unaweza pia kuuza simu used au mpya.
Faida: Vifaa hivi vina faida kubwa, na mauzo ya kila siku ni makubwa. Duka moja linaweza kuuza bidhaa zenye jumla ya faida zaidi ya TZS 100,000 kwa siku.
Mtaji wa kuanzia: TZS 1,000,000 – 5,000,000
7. Biashara ya Usafirishaji (Bodaboda, Bajaji, Delivery Services)
Ikiwa una bajaji au bodaboda yenye leseni, unaweza kuifanya kazi ama mwenyewe au ukaajiri dereva.
Faida: Bajaji inayofanya kazi kwa bidii maeneo ya mjini inaweza kuleta faida ya kati ya TZS 50,000 – 150,000 kwa siku.
Mtaji wa kuanzia: TZS 3,000,000 – 10,000,000 (kwa gari au bajaji mpya)
Biashara Nyingine Zenye Faida ya TSZ 100,000 kwa Siku
1. Huduma za Urembo (Beauty Salon).
2. Uuzaji wa Vinywaji Baridi (Cold Drinks).
3. Kuuza Vifaa vya Majumbani.
4. Biashara ya Huduma za Usafi (Cleaning Services).
5. Uuzaji wa Bidhaa za Kilimo kama Mbegu na Dawa za Kilimo.
6. Huduma za Usafirishaji kwa Matukio (Event Transport).
7. Kukodisha Vifaa vya Matukio (Event Equipment Rentals).
8. Huduma ya Ukarabati wa Vifaa vya Simu na Kompyuta.
9. Biashara ya Duka la Vyakula vya Haraka (Fast Food).
10. Uuzaji wa Vifaa vya Michezo.
Mbinu za Kuifikia Faida ya Laki Moja kwa Siku
Fanya biashara kwenye eneo lenye mzunguko wa watu wengi – kama stendi, ofisi, shule au masoko.
Toa huduma bora na ya kipekee – wateja warudi.
Tumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako – hasa Instagram, WhatsApp, TikTok.
Wekeza kwenye ubora wa bidhaa au huduma – hakikisha mteja anapata thamani halisi.