Watu wengi hufikiri kwamba huwezi kuanza biashara bila kuwa na mtaji mkubwa, lakini ukweli ni kwamba hata kwa Tsh 50,000 tu, unaweza kuanzisha biashara halali, inayoweza kukuletea faida nzuri kila siku. Kinachohitajika ni ubunifu, uthubutu, na kujua wapi pa kuanzia.
1. Uuzaji wa Vitafunwa Mtaani (Mandazi, Chapati, Vitumbua)
Vitafunwa vina soko kubwa asubuhi na jioni kwenye maeneo ya makazi, shule na stendi.
Mtaji: TZS 20,000 – 50,000
Faida: Ukitengeneza vitafunwa 100 ukauza kwa TZS 500 kila kimoja, unaweza kupata hadi TZS 50,000 kwa siku
Siri: Ladha nzuri + usafi + bei nafuu
2. Uuzaji wa Juisi Asilia kwenye Chupa (Embe, Nanasi, Miwa, Tango)
Juisi asilia ni bidhaa inayopendwa sana, hasa kwenye jua kali.
Mtaji: TZS 30,000 – 50,000
Faida: Juisi chupa 1 ya 500ml huuzwa TZS 1,000 – 2,000. Ukitengeneza 30 chupa, unaweza kupata TZS 60,000
Mahitaji: Blender, chupa tupu, matunda
3. Uuzaji wa Chipsi Ndogo Ndogo (Chipsi Kavu au za Mtaa)
Biashara hii ni rahisi na ina faida nzuri maeneo ya stendi, shule au mitaani.
Mtaji: TZS 30,000 – 50,000
Faida: Faida ya kila sahani ya chipsi inaweza kuwa TZS 300 – 700
Unachohitaji: Viazi, mafuta, chumvi, jiko la mkaa/gas, karatasi za kufungia
Soma Hii : Biashara Ya Mtaji Mdogo Yenye Faida Kubwa Tanzania
4. Uuzaji wa Miwa au Tikitimaji kwa Vipande
Watu wengi hupenda matunda haya kama “snack” ya haraka na baridi.
Mtaji: TZS 20,000 – 50,000
Faida: Faida ya kila kipande inaweza kuwa TZS 200 – 500
Vidokezo: Uuze maeneo ya sokoni au barabarani (sehemu zenye watu wengi)
5. Biashara ya Mkaa wa Rejareja
Nunua debe moja au mbili, kisha uuze kwa vifurushi vidogo (vikopo au plastiki ndogo).
Mtaji: TZS 40,000 – 50,000
Faida: Unaweza kupata faida ya TZS 15,000 – 30,000 kwa debe moja
Wateja: Wakazi wa maeneo ya nyumba za kupanga au vijijini
6. Uuzaji wa Vitu vidogo vya Nyumbani (Sindano, Uzi, Viberiti, Sabuni, Miswaki)
Hizi bidhaa huwa na mzunguko mkubwa – zinaisha kila siku na kila mtu anazitumia.
Mtaji: TZS 30,000 – 50,000
Faida: Faida ya bidhaa moja ni TZS 100 – 300, lakini kwa wingi faida hujikusanya haraka
Ushauri: Ziuze mtaani au mlango kwa mlango kama biashara ya rejareja ya kuhamahama
7. Uuzaji wa Mitumba Midogo Midogo (Skafu, Soksi, Chupi, T-Shirt)
Unaweza kwenda Kariakoo au soko la Karume, ununue kifurushi cha skafu au soksi kisha uuuze kwa rejareja.
Mtaji: TZS 30,000 – 50,000
Faida: Kipande cha TZS 1,000 unaweza kuuza kwa TZS 2,000 – 3,000
Siri: Kuwa mbunifu kwenye uuzaji – tumia WhatsApp, marafiki na jamaa
8. Biashara ya Aksesari za Kike (Hereni, Bangili, Mikufu)
Wanawake hupenda kujipamba kila siku. Nunua kwa jumla, uza kwa bei ya rejareja.
Mtaji: TZS 30,000 – 50,000
Faida: Kila kipande kinaweza kuleta faida ya TZS 500 – 2,000
Mahali pazuri: Vyuoni, kazini, au mitandaoni
9. Kupika na Kuuza Karanga, Njugu au Ufuta
Hizi ni bidhaa za kudumu na hupendwa na watu wengi kwa vitafunwa.
Mtaji: TZS 20,000 – 50,000
Faida: Kilo 1 ya karanga inaweza kugawanywa na kuuzwa kwa faida ya TZS 10,000+
Mbinu: Panga vifurushi vya TZS 200, 500 na 1000
10. Biashara ya Uuzaji wa Vocha au Miamala ya Simu (Ageni/Line Agent)
Kama uko maeneo yenye watu wengi, unaweza kufanya biashara ya vocha au miamala midogo ya simu.
Mtaji: TZS 50,000
Faida: Komisheni ndogo ndogo kwa kila muamala, lakini ukipata wateja wengi, inalipa
Vidokezo: Jiunge na mitandao kama M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money nk
Vidokezo vya Mafanikio kwa Mtaji Mdogo:
Anza kidogo lakini kwa malengo makubwa
Hudumia vizuri kila mteja – kila mteja ni kama dhahabu
Tumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako hata kama ni ndogo
Rudia faida na ongeza bidhaa polepole – biashara inakua kwa hatua