Leseni ya udereva ni nyaraka muhimu kwa mtu yeyote anayetaka kuendesha gari kihalali nchini Tanzania. Kuna aina mbalimbali za leseni pamoja na ada zinazohusiana nazo, kulingana na daraja na muda wa leseni husika.
Aina za Madaraja ya Leseni za Udereva nchini Tanzania
Tanzania ina madaraja mbalimbali ya leseni za udereva, kila moja ikiruhusu kuendesha aina maalum ya chombo cha moto:
Daraja A: Kwa waendesha pikipiki na vyombo vingine vya magurudumu mawili au matatu.
Daraja B: Kwa magari madogo ya abiria yenye uzito usiozidi tani 3.5.
Daraja C: Kwa magari makubwa ya mizigo na mabasi.
Madaraja mengine: Kuna madaraja maalum kama D, E, na F kwa ajili ya magari maalum au kazi maalum.
Ada za Leseni ya Udereva
Ada za leseni ya udereva hutofautiana kulingana na aina ya leseni na huduma inayohitajika. Hapa chini ni muhtasari wa ada hizo:
Leseni ya Muda (Provisional License): Hii ni leseni ya muda inayotolewa kwa wanafunzi wa udereva kabla ya kupata leseni kamili. Ada yake ni Tsh 10,000 na inakuwa halali kwa miezi mitatu.
Ada ya Mtihani wa Udereva: Kabla ya kupata leseni kamili, mtahiniwa anapaswa kulipa ada ya mtihani wa udereva ya Tsh 3,000.
Leseni Kamili ya Udereva: Ada ya leseni kamili ni Tsh 70,000.
Mchakato wa Kupata Leseni ya Udereva
Ili kupata leseni ya udereva nchini Tanzania, fuata hatua zifuatazo:
Kupata Leseni ya Muda (Provisional License):
Jaza fomu ya maombi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Lipa ada ya Tsh 10,000 kwa leseni ya muda.
Kujifunza Udereva:
Jiandikishe katika shule ya udereva inayotambulika kwa mafunzo ya nadharia na vitendo.
Kufanya Mtihani wa Udereva:
Baada ya mafunzo, fanya mtihani wa udereva na ulipe ada ya mtihani ya Tsh 3,000.
Kupata Leseni Kamili:
Ukipasi mtihani, lipa ada ya leseni kamili ya Tsh 70,000 ili upate leseni yako.