Kila siku tunatumia Nishati ya umeme majumbani kwetu au viwandani kwene shughuli zetu za kila siku lakini wengi wetu linapokuja kwenye swala la gharama tunakuwa sio wafuatiliai wa gharama husika hasa kujua gharama ya kila unit moja tunayoitumia kupitia Makala hii tunakusanua kuhusu bei ya unit moja.
Bei za Umeme kwa Makundi Mbalimbali ya Wateja (Unit Moja ya Umeme Shilingi Ngapi)
Kwa mujibu wa Sheria ya EWURA, Sura ya 414, na Sheria ya Umeme, Sura ya 131, bei za umeme nchini Tanzania zimeidhinishwa na EWURA na ni kama ifuatavyo:
D1: Wateja wa Majumbani
- Bei ya Nishati (0 – 75 kWh): TZS 100 kwa kWh
- Bei ya Nishati (Zaidi ya 75 kWh): TZS 350 kwa kWh
Wateja hawa ni wale wanaotumia wastani wa unit 75 kwa mwezi. Matumizi yatakayozidi unit 75 yatatozwa bei ya juu ya TZS 350 kwa kila unit inayozidi. Umeme unatolewa katika msongo mdogo wa umeme kwenye njia moja (230V).
T1: Wateja wa Kawaida
- Bei ya Nishati: TZS 292 kwa kWh
Wateja hawa ni pamoja na wateja wa majumbani, biashara ndogondogo, viwanda vidogo, taa za barabarani, na mabango. Umeme unatolewa katika msongo mdogo wa umeme kwenye njia moja (230V) na njia tatu (400V).
T2: Wateja wa Matumizi Makubwa
- Bei ya Nishati: TZS 195 kwa kWh
- Tozo ya Huduma: TZS 14,233 kwa mwezi
- Bei ya Mahitaji ya Juu: TZS 15,004 kwa kVA/Mwezi
Wateja hawa ni wale wenye matumizi ya kawaida ya umeme kupitia 400V na matumizi kwa mwezi ni zaidi ya unit 7,500.
T3-MV: Wateja wa Msongo wa Kati
- Bei ya Nishati: TZS 157 kwa kWh
- Tozo ya Huduma: TZS 16,769 kwa mwezi
- Bei ya Mahitaji ya Juu: TZS 13,200 kwa kVA/Mwezi
Wateja hawa wameunganishwa katika msongo wa kati wa umeme (Medium Voltage).
T3-HV: Wateja wa Msongo Mkubwa
- Bei ya Nishati: TZS 152 kwa kWh
- Bei ya Mahitaji ya Juu: TZS 16,550 kwa kVA/Mwezi
Wateja hawa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement, ambao wameunganishwa katika msongo mkubwa wa umeme (High Voltage).
Umeme wa 5000 ni Unit Ngapi?
Ili kuelewa vizuri jinsi bei ya umeme inavyopimwa, ni muhimu kujua umeme wa kiasi fulani wa fedha ni sawa na unit ngapi.
Kwa mfano, kwa wateja wa kundi la D1, umeme wa TZS 5000 unaweza kua unit 50 ikiwa matumizi ya mteja yapo chini ya unit 75. Ikiwa matumizi ya mteja yanazidi unit 75, bei itakuwa TZS 350 kwa kWh kwa units zinazozidi.
Umeme wa 1000 ni Unit Ngapi?
Kwa wateja wa kundi la D1, umeme wa TZS 1000 unaweza kutoa unit 10 kwa matumizi ya chini ya unit 75. Ikiwa matumizi ya mteja yanazidi unit 75, basi TZS 1000 itakuwa sawa na takribani unit 2.86 kwa bei ya TZS 350 kwa kWh.