Katika dunia ya kidijitali, njia za kujifunza zimebadilika kwa kasi kubwa. Huna haja tena ya kusafiri kwenda darasani au kusubiri mwalimu ili ujifunze Kiingereza. Kwa simu yako ya mkononi, unaweza sasa kujifunza Kiingereza kwa haraka, kwa ufanisi, na kwa njia ya kufurahisha.
MISINGI YA LUGHA YA KIINGEREZA UKITAKA KUKIJUA HARAKA
Kabla hujapakua app yoyote, ni muhimu kuelewa vipengele vya msingi vya lugha ya Kiingereza ambavyo vinapaswa kupewa kipaumbele ili kujifunza kwa haraka:
Msamiati (Vocabulary) – Jifunze maneno ya kila siku yanayotumika sana.
Sarufi (Grammar) – Fahamu jinsi ya kutengeneza sentensi sahihi.
Matamshi (Pronunciation) – Elewa namna sahihi ya kutamka maneno.
Kusikiliza (Listening) – Sikiliza sauti na mazungumzo ya asili ili kuzoea lafudhi.
Kuandika na Kuzungumza (Writing & Speaking) – Fanya mazoezi ya kuandika na kujieleza kwa maneno yako mwenyewe.
Kwa kutumia app zenye vipengele hivi, utaweza kujifunza Kiingereza kwa haraka zaidi na kwa ufanisi mkubwa.
APP ZA ANDROID NA LINK ZAKE ZA KUJIFUNZA KIINGEREZA KWA HARAKA
Duolingo
Maelezo: Hutoa masomo kwa njia ya michezo na mafupi mafupi. Nzuri kwa wanaoanza.
BBC Learning English
Maelezo: Ina video, masomo ya sarufi, na mazoezi ya kusikiliza.
HelloTalk
Maelezo: Zungumza moja kwa moja na wazungumzaji wa Kiingereza duniani kote.
Link: Pakua HelloTalk
Memrise
Maelezo: Inatumia video halisi za watu wakizungumza, nzuri kwa kujifunza matamshi.
Link: Pakua Memrise
Busuu
Maelezo: Masomo yaliyopangwa kwa ngazi mbalimbali na mitihani ya kujipima.
Link: Pakua Busuu
APP ZA IOS NA LINK ZAKE ZA KUJIFUNZA KIINGEREZA KWA HARAKA
Duolingo
Link: Pakua Duolingo kwa iOS
BBC Learning English
HelloTalk
Link: Pakua HelloTalk kwa iOS
Memrise
Link: Pakua Memrise kwa iOS
Busuu
Link: Pakua Busuu kwa iOS
Soma Hii : Jinsi ya Kujifunza kiingereza kwa haraka zaidi
MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA KUHUSU APP NZURI YA KUJIFUNZA KIINGEREZA KWA HARAKA
1. Ni ipi app bora kabisa ya kujifunza Kiingereza?
App bora hutegemea kiwango chako na malengo yako. Duolingo ni nzuri kwa kuanza, lakini Busuu na Memrise hufaa zaidi kwa maendeleo ya haraka.
2. Je, apps hizi ni bure?
Nyingi zina matoleo ya bure, lakini pia zinatoa matoleo ya kulipia ili kupata vipengele zaidi.
3. Je, ninaweza kujifunza Kiingereza bila kwenda darasani?
Ndiyo. Ukiwa na nidhamu, app nzuri, na muda wa kujifunza kila siku, unaweza kujifunza Kiingereza kikamilifu bila darasa la kawaida.
4. App hizi zinahitaji intaneti?
App nyingi kama Duolingo na Memrise hutoa sehemu ya kujifunza nje ya mtandao (offline) endapo utapakua masomo mapema.
5. Je, apps hizi zinafundisha matamshi sahihi?
Ndio, hasa Memrise na BBC Learning English zinajikita zaidi kwenye matamshi na mazungumzo halisi.