Anemia ni hali ya kiafya inayotokea pale ambapo mwili hauna seli nyekundu za damu za kutosha au hauna kiwango cha kutosha cha hemoglobini. Hemoglobini ni protini muhimu kwenye seli nyekundu za damu inayobeba oksijeni kutoka kwenye mapafu na kuisambaza mwilini kote. Wakati seli hizi hazipo kwa wingi au hazifanyi kazi ipasavyo, mwili hupata upungufu wa oksijeni na kusababisha dalili mbalimbali kama uchovu, udhaifu na ngozi kuwa ya rangi ya kijivu au kupauka.
Sababu Kuu za Anemia
Upungufu wa madini chuma (Iron deficiency anemia)
Hii ndiyo aina ya anemia inayopatikana zaidi. Inatokea pale mwili unapopata chuma kidogo kupitia chakula au unashindwa kukitumia ipasavyo kutengeneza hemoglobini.Upungufu wa vitamini
Vitamini B12 na folic acid ni muhimu katika kutengeneza seli nyekundu za damu. Upungufu wake unaweza kusababisha aina ya anemia inayoitwa megaloblastic anemia.Kupoteza damu kwa wingi
Kupoteza damu kutokana na ajali, upasuaji, hedhi nzito kwa wanawake, au kutokwa na damu ndani kwa ndani (mfano kutokana na vidonda vya tumbo) kunaweza kusababisha anemia.Magonjwa sugu
Baadhi ya magonjwa sugu kama vile saratani, maambukizi ya muda mrefu, au magonjwa ya figo yanaweza kuathiri uwezo wa mwili kutengeneza seli nyekundu za damu.Urithi (genetic factors)
Kuna aina fulani za anemia ambazo zinasababishwa na kurithi vinasaba, kama vile sickle cell anemia na thalassemia, ambazo huathiri namna seli nyekundu zinavyoundwa na kufanya kazi.Mambo ya lishe duni
Kula chakula kisicho na madini na vitamini muhimu kwa afya ya damu, kwa mfano lishe isiyo na nyama, mboga za kijani, nafaka kamili na matunda, inaweza kuchangia anemia.Matatizo ya uboho wa mifupa
Uboho wa mifupa ndiyo huchakata na kuzalisha seli mpya za damu. Magonjwa kama leukemia au saratani nyingine za uboho huzuia uzalishaji wa kutosha wa seli nyekundu.