Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatoa vifurushi mbalimbali vya bima ya afya kwa mtu binafsi, vikiwa na lengo la kukidhi mahitaji tofauti ya kiafya na uwezo wa kifedha wa wanachama. Fahamu Aina ya Vifurushi Vya Bima ya Afya NHIF kwa Mtu Binafsi na Gharama zake.
Aina ya Vifurushi Vya Bima ya Afya NHIF kwa Mtu Binafsi

Serengeti Afya
Kifurushi hiki kinatoa wigo mpana wa huduma za matibabu, ikiwemo:
- Huduma za madaktari wa kawaida, bingwa, na bingwa bobezi.
- Vipimo vya kina kama CT-Scan, MRI, Ultra Sound, na X-ray.
- Matibabu ya magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo.
- Huduma za uzazi, upasuaji mkubwa na mdogo, pamoja na matibabu ya saratani (dawa na mionzi tiba).
- Huduma za meno, utengamao, na vifaa tiba pandikizi.
Ngorongoro Afya
Hiki ni kifurushi kinacholenga huduma za msingi na baadhi ya huduma za kibingwa, ikiwemo:
- Huduma za madaktari wa kawaida na bingwa.
- Vipimo vya maabara, CT-Scan, na Ultra Sound.
- Matibabu ya magonjwa sugu na baadhi ya magonjwa ya saratani.
- Huduma za uzazi na baadhi ya upasuaji mdogo.
Viwango vya Michango kwa Wanachama wa Bimba ya Afya ta NHIF
Kiwango cha mchango kinategemea ukubwa wa familia na kifurushi kinachochaguliwa. Kwa mfano:
- Serengeti Afya: Kuanzia TZS 660,000 kwa mtu mmoja mwenye umri wa miaka 18-35.
- Ngorongoro Afya: Kuanzia TZS 240,000 kwa mtu mmoja mwenye umri wa miaka 0-17.
Jinsi ya Kujisajili na Vifurushi Vya Bima ya Afya NHIF 2024
JJ