Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini Tanzania katika kutoa mafunzo ya usafirishaji, uhandisi wa magari, na masuala mengine ya uchukuzi. Moja ya programu maarufu zinazotolewa na NIT ni mafunzo ya udereva. Ikiwa unatafuta taarifa kuhusu ada na kozi za udereva zinazotolewa na NIT, basi makala hii itakupa mwongozo kamili.
KAda za Kozi ya Udereva Chuo cha NIT
Chuo cha NIT kinatoa kozi mbalimbali za udereva zinazolenga kukidhi mahitaji tofauti ya wanafunzi na madereva. Kozi hizi zinatofautiana kutoka zile za msingi hadi kozi maalum kwa madereva waliobobea.
Zifuatazo ni baadhi ya kozi maarufu za udereva zinazotolewa pamoja na ada kwa kozi husika:
Kozi ya Msingi ya Udereva (Basic Driving Course)
Kozi hii inalenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa msingi kama vile jinsi ya kudhibiti gari na kufuata sheria za barabarani. Ni kozi inayofaa kwa wale wanaoanza safari yao ya udereva.
Ada: TZS 200,000 kwa muda wa siku 11.
Kozi ya Udereva wa Magari Makubwa (Heavy Goods Vehicle – HGV)
Hii ni kozi maalum inayowafundisha madereva jinsi ya kuendesha magari makubwa kama vile malori na magari ya mizigo. Inahitaji ujuzi wa awali wa udereva.
Ada: TZS 515,000 kwa muda wa siku 15.
Kozi ya Madereva wa VIP (Advanced Drivers Grade II – VIP)
Kozi hii inafaa kwa wale wanaotaka kuimarisha ujuzi wao wa udereva, hasa wale wanaoendesha magari kwa viongozi au watu mashuhuri.
Ada: TZS 400,000 kwa muda wa wiki 4.
Kozi ya Udereva wa Gari za Abiria (Passenger Service Vehicle – PSV)
Kozi hii inafundisha jinsi ya kuendesha magari ya abiria kama vile daladala au mabasi. Inalenga madereva wanaotaka kufanya kazi kwenye sekta ya usafiri wa umma.
Ada: TZS 200,000 kwa muda wa siku 11.
Kozi ya Udereva Maalum (Senior Driver Course)
Kozi hii ni maalum kwa madereva wenye uzoefu ambao wanahitaji kuongeza maarifa ya hali ya juu katika udereva wa magari maalum au magari ya mizigo.
Ada: TZS 450,000 kwa muda wa wiki 6.
Kozi ya Waendeshaji wa Forklift (Forklift Operator’s Training)
Hii ni kozi kwa ajili ya madereva wa magari ya kuinua mizigo (forklift) inayotumika kwenye viwanda na maghala.
Ada: TZS 400,000 kwa muda wa siku 5.
Wanafunzi wanashauriwa kulipa Ada za Kozi ya Udereva Chuo cha NIT 2024/2025 mapema kabla ya tarehe ya kuanza kozi.
Malipo yote yanafanywa kupitia mfumo wa serikali wa GePG kwa kutumia namba maalum ya malipo (Control Number) ambayo hutolewa na chuo. Gharama za kozi zinajumuisha mafunzo yote lakini washiriki watajitegemea kwa malazi na chakula.
Maelezo ya Mawasiliano
Kwa maelezo zaidi au maswali kuhusu ada za mafunzo ya udereva, unaweza kuwasiliana na ofisi ya udahili kupitia:
Simu: +255 22 2400148/9
Fax: +255 22 2443140
Simu ya Mkononi:
+255 684 757 774
+255 762 202 215
+255 713 794 870
+255 782 422 199
Barua pepe: admission@nit.ac.tz