Kila mwaka, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) hutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu katika awamu tofauti. Baada ya kutangazwa kwa awamu ya kwanza, wanafunzi waliokosa nafasi au waliochelewa kuomba hupata fursa ya kuchaguliwa katika awamu ya pili. Kwa mwaka wa masomo wa 2025, TCU na vyuo vikuu mbalimbali vimetoa orodha ya wanafunzi waliopata nafasi katika awamu hii.
Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali tarehe 05 Oktoba, 2025. Wanafunzi wanatakiwa kuthibitisha udahili wao kuanzia tarehe hiyo hadi 21 Oktoba, 2025, ili kudumisha nafasi zao.
Ni muhimu kufahamu kwamba kushindwa kuthibitisha udahili ndani ya muda uliowekwa kunaweza kusababisha kupoteza nafasi hiyo na kupewa mwanafunzi mwingine ambae amekosa nafasi katika dirisha la pili la udahili wa vyuo.
Waombaji Waliodahiliwa katika Chuo Zaidi ya Kimoja
Wanafunzi ambao wamechaguliwa kujiunga na vyuo zaidi ya kimoja wanatakiwa kuchagua chuo kimoja na kuthibitisha udahili wao. Hii itafanyika kupitia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) au barua pepe. Wale ambao hawataweza kupata ujumbe huo wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa ili kupata namba hiyo ya siri.
Kwa taarifa zaidi, wanafunzi wanaweza kutembelea tovuti rasmi ya TCU ili kupata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa katika chuo zaidi ya kimoja Au Soma zaidi kupitia chapisho letu hili
Awamu ya Tatu ya Udahili wa vyuo Vikuu
Baada ya kukamilika kwa awamu mbili za udahili, TCU imeamua kufungua Awamu ya Tatu ya udahili itakayoanza ,2025. Hii ni fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kupata udahili katika awamu zilizopita. Vyuo vinaelekezwa kutangaza programu ambazo bado zina nafasi ili kuwapa waombaji nafasi ya kujiunga.
SOMA HII :Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu UDSM 2025/2026
Njia za Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili
Wanafunzi wanapaswa kufuatilia kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa kwa karibu. Hapa kuna njia kuu za kuangalia majina haya:
- Kupitia Tovuti ya TCU: Tembelea tovuti rasmi ya TCU www.tcu.go.tz ili kuona orodha ya vyuo vilivyopokea udahili na majina ya wanafunzi waliochaguliwa.
- Tovuti za Vyuo Vikuu: Kila chuo kikuu kitakuwa na orodha ya wanafunzi waliochaguliwa katika tovuti yake. Ni muhimu kuhakikisha kuwa taarifa zote ni sahihi.
- Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS): Wanafunzi wanaweza kupokea ujumbe mfupi kuwajulisha kuhusu udahili wao na hatua zinazofuata.
- Mfumo wa Maombi ya Mtandaoni: Wanafunzi wanaweza pia kuangalia majina yao kupitia mfumo wa maombi wa mtandaoni kwa kuingia katika akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba.