University of Dar es salaam (UDSM) Kila mwaka, hupokea maelfu ya maombi kutoka kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu mbalimbali za masomo. Kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026, UDSM imetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika awamu ya kwanza.
Kuhusu Chuo kikuu Dar es salaam (UDSM)
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD) (kiingereza: University of Dar es Salaam) ni chuo kikuu cha kwanza nchini Tanzania chenye kauli mbinu inayosema Hekima ni Uhuru. CKD kina kampasi mbalimbali kama vile Main Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi, MUCE Kampasi, Zanzibar Kampasi, SJMC Kampasi na Mbeya Kampasi. Hizi Kampasi zipo mahali mbalimbali. Main Kampasi, CoICT Kampasi, DUCE Kampasi na SJMC Kampasi zinapatikana jijini Dar es Salaam. MUCE Kampasi inapatikana mkoa wa Iringa. Zanzibar Kampasi inapatikana Zanzibar. Mbeya Kampasi inapatikana jijini Mbeya.
Jinsi ya Kuangalia kama Umechaguliwa Chuo kikuu UDSM
Kwa wale walioomba kujiunga na chuo cha UDSM mwaka 2025, kuna njia mbili kuu za kuangalia kama wamechaguliwa:
1. Kupitia Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS)
- UDSM itatuma SMS kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenye namba za simu walizotumia wakati wa kutuma maombi ya kujiunga na chuo.
- Ujumbe huu utakuwa na maelezo muhimu, ikiwa ni pamoja na kozi ambayo mwanafunzi amechaguliwa
- Hakikisha namba yako ya simu inafanya kazi na ipo sehemu yenye mtandao wa kutosha kupokea ujumbe.
Kama hujapokea SMS kufikia tarehe ya mwisho ya kuthibitisha udahili, tumia njia ya pili (online) kuangalia kama umechaguliwa.
2. Kutumia Mfumo wa Maombi ya Mtandaoni (Online Admission System)
- Tembelea tovuti rasmi ya UDSM OAS (https://admission.udsm.ac.tz/).
- Tafuta sehemu ya “Admissions” au “Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa”.
- Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilounda wakati wa kuomba.
- Mara baada ya kuingia, utaona ujumbe unaoonyesha kama umechaguliwa au la.Kama umechaguliwa, utaona maelezo ya kozi uliyopangiwa.
- Ili kuthibitisha udahili wako, utahitajika kuingiza msimbo maalum (SPECIAL CODE) utakaotumwa kwako kwa njia ya SMS.
SOMA HII :Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa Chuo Kikuu Dodoma UDOM
Mambo ya Kuzingatia kwa Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025
Hongera sana kama umechaguliwa kujiunga na UDSM! Lakini safari yako haishii hapo. Hapa kuna hatua muhimu unazopaswa kuchukua:
- Thibitisha Udahili Wako: Hakikisha unathibitisha udahili wako kabla ya tarehe ya mwisho iliyoainishwa na UDSM. Kutothibitisha kunaweza kusababisha nafasi yako kupewa mwanafunzi mwingine.
- Soma kwa Makini Fomu za Kujiunga: UDSM itatoa fomu za kujiunga ambazo utahitajika kuzijaza na kuzirejesha. Soma fomu hizi kwa makini na uhakikishe unatoa taarifa sahihi.
- Lipa Ada na Gharama Nyingine: UDSM itatoa maelezo kuhusu ada ya masomo na gharama nyingine zinazohitajika. Hakikisha unalipa ada kwa wakati ili kuepuka matatizo yoyote.
- Jiandae kwa Maisha ya Chuo Kikuu: Maisha ya chuo kikuu ni tofauti na maisha ya shule ya sekondari. Jiandae kwa changamoto mpya na fursa nyingi za kujifunza na kukua.