Chuo kikuu Dodoma Tayari kimeshamaliza Mchakato wa Udahili na kutoa Majina ya Waliochaguliwa UDOM Kwa mwaka wa Masomo 2025 ,Kama unatafuta majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa mwaka wa masomo 2025 /2026 Fuata hatua zifuatazo.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa UDOM
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni moja ya taasisi kubwa za elimu ya juu nchini Tanzania, kinachotoa programu mbalimbali kwa wanafunzi wa shahada na ngazi nyingine za elimu. Kila mwaka, UDOM hupokea maelfu ya maombi kutoka kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hiki. Kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026, chuo kimetangaza rasmi majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika awamu ya kwanza.
1. Kupitia Ujumbe Mfupi wa Simu
Wanafunzi waliochaguliwa watapokea ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kutoka UDOM kwenye namba za simu walizotumia wakati wa kuomba. Ujumbe huo utakuwa na maelezo kuhusu kozi ambayo mwanafunzi amechaguliwa.
2. Kutumia Mfumo wa UDOM OAS (Online Admission System)
Tembelea tovuti rasmi ya UDOM OAS kupitia kiunganishi: https://application.udom.ac.tz.
Bonyeza kitufe cha “LOGIN” na ingiza taarifa zako za akaunti (Username na Password) ambazo ulitumia wakati wa kutuma maombi.
Baada ya kuingia kwenye akaunti yako, utaona ujumbe unaokujulisha kama umechaguliwa, pamoja na maelezo ya kozi uliyochaguliwa. Ili kuthibitisha udahili wako, utaingiza SPECIAL CODE utakayotumiwa kwa SMS.
Kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Chuo Kikuu cha Dodoma kilianzishwa mwaka 2007 na ni chuo kikuu kikubwa zaidi nchini Tanzania, kikiwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi wapatao 40,000 pindi miundombinu yake itakapokamilika. UDOM inajivunia kujengwa kwa kutumia fedha za ndani, ikiwa na dhamira ya kuchangia maendeleo ya Tanzania na dunia kwa ujumla.
Chuo hiki kipo katikati ya nchi, ndani ya jiji la Dodoma, na kinatoa fursa kwa wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje. UDOM inatoa programu mbalimbali za masomo zenye viwango tofauti, zikiwemo za Afya, Uhandisi, Elimu, Teknolojia, Biashara, Sanaa, na Sheria, miongoni mwa zingine. Pia, chuo kina vyuo na taasisi tofauti ambazo zimejengwa kwa ajili ya kutoa huduma maalum kwa wanafunzi.
Hatua za Kuchukua Baada ya Kuchaguliwa
Ikiwa umechaguliwa kujiunga na UDOM, kuna hatua muhimu unazopaswa kuchukua ili kukamilisha usajili wako:
- Pakua Barua ya Udahili
- Hakikisha unapakua barua yako ya udahili kutoka kwenye tovuti ya chuo.
- Lipia Ada za Awali
- Jifunze kuhusu ada zinazotakiwa na hakikisha unalipa kiasi kinachohitajika kwa wakati.
- Jiandae kwa Safari ya Masomo
- Kama unatoka nje ya Dodoma, anza kufanya maandalizi ya safari yako kuelekea chuoni.
- Jiunge na Makundi ya Wanafunzi
- Jiunge na vikundi vya mitandao ya kijamii vya wanafunzi wa UDOM ili kupata taarifa muhimu.
SOMA HII :Heslb :Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 Awamu Ya Kwanza
Wasiliana na UDOM Moja kwa Moja
- Ikiwa hupati majina kwenye tovuti, unaweza kuwasaidia UDOM moja kwa moja kupitia:
- Simu: +255 26 231 0010
- Barua pepe: info@udom.ac.tz
- Ofisi za UDOM: Tembelea chuo hicho kwa msaada wa moja kwa moja.