Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa tangazo rasmi la ajira mpya tarehe 3 Juni 2025. Fursa hizi ni kwa Watanzania wenye sifa stahiki, walio tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini.
Tangazo hili linatoa nafasi mbalimbali za ajira kwa kada tofauti, zikiwa na sifa na majukumu tofauti. Hii ni fursa adhimu kwa wale wanaotamani kuwa sehemu ya chombo muhimu cha utoaji haki nchini.
Orodha ya Nafasi Zilizotangazwa
Kada | Nafasi | Kituo cha Kazi | Closing Date | ||
---|---|---|---|---|---|
1 | CIVIL TECHNICIAN II (CARPENTER) | Nafasi 3 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 |
2 | CIVIL TECHNICIAN II (PAINTER) | Nafasi 3 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
3 | TECHNICIAN II (ELECTRICAL) | Nafasi 4 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
4 | TECHNICIAN II (PLUMBING) | Nafasi 6 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
5 | TECHNICIAN II (AIR CONDITION (HVAC) | Nafasi 10 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
6 | TECHNICIAN II (WELDING AND FABRICATION TECHNICIAN) | Nafasi 2 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
7 | MSAIDIZI WA OFISI | Nafasi 42 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
8 | MLINZI | Nafasi 3 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
9 | DEREVA II | Nafasi 33 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
10 | MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II | Nafasi 46 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
11 | AFISA MWENDESHA OFISI DARAJA II | Nafasi 5 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
12 | MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II | Nafasi 80 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
13 | MPISHI | Nafasi 8 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
14 | MSAIDIZI WA MAKTABA II | Nafasi 5 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
15 | MKUTUBI II | Nafasi 2 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
16 | OPERETA WA KOMPYUTA MSAIDIZI | Nafasi 8 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
17 | OPERATA WA KOMPYUTA II | Nafasi 5 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
18 | MSAIDIZI WA HESABU II | Nafasi 10 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
19 | AFISA UTUMISHI II | Nafasi 10 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 | |
20 | HAKIMU MKAZI II | Nafasi 46 | Mahakama ya Tanzania | Tuesday 17 June 2025 |
[Soma: Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Ajira Portal, Serikalini na UTUMISHI 2025 ]
Maelekezo Muhimu kwa Waombaji
Maombi yote yatumwe kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama: www.jsc.go.tz
Mwisho wa kutuma maombi: Tarehe 17 Juni, 2025
Waombaji wote lazima:
Wasilishe vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, picha (passport size), NIDA
Watie maelezo sahihi – taarifa za uongo zitapelekea kufukuzwa kazi
Wale waliopata ajira ya kudumu serikalini hawaruhusiwi kuomba
Wenye ulemavu wapewe kipaumbele – waeleze aina ya ulemavu wao
Umri wa kuomba: Miaka 18 hadi 45
Kwa maelezo zaidi:
Simu: 0734 219 821 au 0738 247 341
Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz