Kumtongoza msichana uliyempenda kwa mara ya kwanza ni kitu kinachohitaji uangalifu, hekima, na uhalisia. Mara nyingi, hisia za kimapenzi zinapotokea kwa mara ya kwanza, zinaweza kufanya mtu ajisikie kuwa hajui jinsi ya kuanza. Hata hivyo, kwa kutumia mbinu sahihi na maneno makini, unaweza kumvutia na kumfanya ajisikie kuwa anapendwa na kuthaminiwa. Hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kumtongoza msichana uliyempenda kwa mara ya kwanza:
Angalia usafi wako.
Kabla hujachukua hatua yeyote ya kuongea na mwanamke hakikisha kuwa uko nadhifu. Kwanza piga mswaki, valia nguo safi na pia ukiwa na marashi jipulize. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa mchafu basi hakuna mwanamke yeyote atakubali kuongea nawe.
Pia hakikisha unapoamua kumuapproach unaangalia nguo ulizovalia. Je, nguo umevalia kinamna gani. Huwezi kuapproach mwanamke uongee naye katika klabu wakati umevalia kana kwamba unaenda kwa ibada. Hakikisha kuwa nguo zako unazozivaa zina wiana na mazingira ulipo.
Muapproach ukiwa anakuona.
Wakati unamuapproach mwanamke huyu hakikisha tayari amekuona. Usimuapproach kama mwizi. Nenda moja kwa moja sehemu ambayo yuko huku ukionyesha tabasamu la kuwa uko tayari kuongea na yeye pindi ambapo utamfikia.
Tabasamu.
Kama nilivyotangulia kusema ya kuwa lazima uwe unatabasamu ukiwa unaaproach mwanamke, hivyo hivyo ni muhimu kutabasamu wakati umekaa kando ya mwanamke. Hii ni muhimu kwa kuwa utamfanya mwanamke huyu kujihisi huru mbele yako na pia ni njia moja wapo ya kujitokeza kirafiki.
Mwangalie machoni.
Ushamfikia huyu mwanamke. Kitu ambacho kinafuatia ni lazima uonyeshe ujasiri. Na ujasiri wako utaonekana pale ambapo utamwangalia huyu mwanamke machoni. Ukiwa unaanza mazungumzo na yeye, haupaswi kuangalia upande ama kuangalia chini.
Tumia ishara za mikono.
Kutumia mikono yako mara kwa mara kuashiria kitu ama jambo fulani kunakupa ujasiri wa ghafla. Pia matumizi ya ishara hizi husaidia kusisitiza jambo fulani kando na kuwa inakupatia utulivu wakati mazungumzo yenu yanaendelea.
Tumia sauti na lugha inayofaa.
Ukiongea kwa sauti kubwa na mwanamke basi utampa ishara ya kuwa wewe ni duko, yaani masikio yako ni mazito. Ukiongea haraka haraka atakuona wewe ni mjinga. Pia ukiongea kwa sauti laini atakuona wewe hujakomaa na hufanani na mwanaume thabiti. So hapa lazima ujifundishe jinsi ya kuongea na mwanamke vile inavyotakikana.
Hali kadhalika, matumizi ya lugha yako ni muhimu. Usitumie lugha ya kudhalilisha mtu, usitumie matusi, usitumie lugha ya uchafu. Yaani hapa lazima uwe mstaarabu kwa kuwa ni mara ya kwanza kwako kuongea na huyu mwanamke.
SOMA HI :Maneno mapya unayopaswa kuyatumia wakati wa kutongoza
Msifu.
Hii ni mbinu moja wapo ya kumfanya mwanamke ajiskie huru na kujiona kuwa angalau ameweza kumzuzua mwanaume. Kujipodoa lisaa lizima asubuhi hakuji hivi hivi!
Ingiza ucheshi ndani ya mazungumzo.
Wakati unaendelea kuongea na mwanamke huyu, hakikisha ya kuwa unaingiza ucheshi ndani ya mazungumzo yako. Hii ni muhimu kwa kuwa wanawake huvutiwa na wanaume ambao ni wacheshi.
Tumia Maneno Matamu na ya Kufanya Ajisikie Muhimu
Maneno matamu yana nguvu kubwa katika kumtongoza msichana. Tumia maneno yanayomfanya ajisikie kuwa ana thamani na kuwa wa pekee. Kwa mfano:
- “Unaipa maisha yangu maana.”
- “Sijui nitakua vipi bila wewe.”
- “Uko kwenye akili zangu kila wakati.”
Maneno kama haya yanaweza kumfanya ajisikie kuwa anapendwa na kuthaminiwa.