Madini ya chuma ni kirutubisho muhimu sana kwa afya ya mwili wa binadamu. Yanahitajika katika kutengeneza hemoglobini – protini inayopatikana kwenye seli nyekundu za damu na inayosaidia kubeba oksijeni kutoka kwenye mapafu kwenda kwenye sehemu zote za mwili. Ukosefu wa madini haya unaweza kuathiri kwa kiwango kikubwa ustawi wa mwili na kusababisha matatizo ya kiafya.
Ukosefu wa Madini ya Chuma Husababisha Ugonjwa Gani?
Ukosefu wa madini ya chuma husababisha ugonjwa uitwao Upungufu wa damu kwa sababu ya ukosefu wa madini ya chuma, kitaalamu unajulikana kama Iron Deficiency Anemia.
Ugonjwa huu hutokea pale mwili unaposhindwa kutengeneza kiwango cha kutosha cha seli nyekundu za damu zenye hemoglobini ya kutosha, kutokana na uhaba wa madini ya chuma.
Dalili za Iron Deficiency Anemia
Kelele masikioni (tinnitus)
Uchovu wa mara kwa mara
Kizunguzungu au kuishiwa nguvu
Upungufu wa pumzi hata bila kazi ngumu
Moyo kwenda mbio
Ngozi kuwa ya rangi ya kijivu au weupe usio wa kawaida
Kichwa kuuma mara kwa mara
Kukosa hamu ya kula (hasa kwa watoto)
Kukatika kwa nywele au kuchanika kwa kucha kirahisi
Kukosa uwezo wa kujifunza kwa watoto
Sababu Zinazochangia Ukosefu wa Madini ya Chuma
Lishe duni isiyo na vyakula vyenye chuma.
Kupoteza damu kwa wingi, mfano kutokana na hedhi nzito au ajali.
Ujauzito – mahitaji ya chuma huongezeka kwa ajili ya mtoto.
Matatizo ya utumbo yanayozuia ufyonzaji wa madini ya chuma.
Kuwepo kwa minyoo tumboni – hasa kwa watoto.
Matumizi ya dawa fulani zinazopunguza ufyonzaji wa chuma mwilini.
Makundi Yaliyo Katika Hatari Zaidi
Wanawake wajawazito
Watoto wachanga na wanaokua haraka
Watu wenye lishe duni
Watu waliopoteza damu kwa upasuaji, hedhi, au ajali
Wagonjwa wa figo au saratani
Matokeo ya Kudumu Iwapo Ugonjwa Hautatibiwa Mapema
Kudhoofika kwa mfumo wa kinga
Kushuka kwa kiwango cha maendeleo ya kiakili kwa watoto
Uchovu sugu na kushuka kwa uwezo kazini au darasani
Kuongezeka kwa hatari ya matatizo wakati wa kujifungua
Jinsi ya Kuzuia na Kutibu Ukosefu wa Madini ya Chuma
1. Kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi:
Nyama nyekundu (nyama ya ng’ombe, maini)
Samaki na dagaa
Mboga za majani (mchicha, kisamvu)
Maharagwe, dengu, choroko
Juisi ya beetroot
Tende, embe, mapera
2. Tumia virutubisho vya chuma kama ulivyoelekezwa na daktari
3. Kunywa matunda yenye vitamini C (kama machungwa, mapera) ili kusaidia mwili kufyonza chuma zaidi
4. Epuka kahawa na chai mara baada ya kula – hupunguza ufyonzaji wa chuma [Soma: Vyakula vyenye madini ya chuma kwa mama mjamzito ]
FAQs – Maswali ya Kawaida Kuhusu Ukosefu wa Madini ya Chuma
1. Je, upungufu wa chuma unaweza kusababisha kifo?
Ndiyo, ikiwa haujatibiwa kwa muda mrefu, unaweza kusababisha matatizo ya moyo na kifo.
2. Je, anemia ni ugonjwa wa kurithi?
Kuna aina fulani za anemia zinazorithiwa, lakini ile inayotokana na ukosefu wa chuma inasababishwa na mazingira au lishe duni.
3. Ni kipimo gani hutumika kugundua ukosefu wa chuma?
Kipimo cha damu kinachoitwa Hemoglobin Test au Full Blood Count (FBC).
4. Ni dawa gani nzuri ya kuongeza madini ya chuma?
Vidonge vya iron kama ferrous sulfate, pamoja na chakula chenye madini ya chuma.
5. Ni chakula gani kinachoongeza chuma haraka?
Maini ya ng’ombe, nyama nyekundu, dagaa, na juice ya beetroot.
6. Ni kwa muda gani mtu huanza kupata nafuu baada ya kutumia dawa za chuma?
Kwa kawaida wiki 2 hadi 4 huanza kuonyesha nafuu ikiwa unatumia dawa na lishe vizuri.
7. Kwa nini wajawazito hupewa vidonge vya chuma?
Kwa sababu mahitaji ya damu huongezeka wakati wa ujauzito ili kusaidia ukuaji wa mtoto.
8. Je, watoto wanaweza kupata anemia?
Ndiyo, hasa kama hawapati lishe bora au wana minyoo.
9. Je, chai huathiri ufyonzaji wa chuma?
Ndiyo, chai na kahawa hupunguza uwezo wa mwili kufyonza chuma.
10. Mboga gani zina chuma nyingi?
Mchicha, kisamvu, majani ya maboga, na spinach.
11. Beetroot ina nafasi gani katika kuongeza chuma?
Ina madini ya chuma na husaidia kuongeza damu mwilini.
12. Je, kunywa maji mengi kunaathiri chuma mwilini?
Hapana, lakini maji ya kisima yenye fluoride nyingi huweza kupunguza ufyonzaji wa chuma.
13. Je, anemia ni dalili ya ugonjwa mkubwa zaidi?
Inaweza kuwa dalili ya matatizo ya utumbo au upungufu wa virutubisho vingine.
14. Ni watu gani wana hatari zaidi ya anemia?
Wajawazito, watoto, watu wenye magonjwa sugu na wanaotoka damu mara kwa mara.
15. Je, upungufu wa damu unaweza kuponwa kabisa?
Ndiyo, iwapo chanzo chake ni ukosefu wa chuma na utazingatia lishe na tiba sahihi.
16. Je, tembele lina chuma?
Ndiyo, ni mboga nzuri ya kuongeza damu.
17. Vidonge vya iron vina madhara?
Wakati mwingine huweza kusababisha kuvimbiwa, kichefuchefu au kinyesi cheusi.
18. Je, mtoto wa mwaka mmoja anaweza kupata upungufu wa damu?
Ndiyo, hasa kama hapewi chakula chenye virutubisho vya kutosha au ana minyoo.
19. Je, sukari inaweza kusababisha upungufu wa damu?
Hapana moja kwa moja, lakini vyakula vyenye sukari nyingi hukosa virutubisho muhimu.
20. Je, damu ya binadamu inaundwa na nini?
Seli nyekundu, seli nyeupe, sahani za damu (platelets), na plasma – seli nyekundu hutegemea chuma ili kufanya kazi.