Chuo cha Maji kina jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalamu wanaotumika na wanao tarajia kutumika katika sekta ya maji, mafunzo yamejikita katika masuala ya ujenzi,ukarabati na matengenezo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira. Mafunzo yanatolewa kwa muda mfupi na muda mrefu. Bofya hapa kusoma zaidi
Majukumu
Majukumu ya Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji ni kama ifuatavyo:
- Kutekeleza shughuli za kiutawala na nyinginezo ili kupata ufanisi katika kutoa mafunzo;
- Kufundisha wataalamu, mafundi sanifu, mafundi bomba kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya maji;
- Kuboresha mitaala na kutengeneza vitendeakazi kwa ajili ya kufundishia karakana na
- Kutunga na kusimamia mitihani na kuhakikisha hakuna uvujaji wa mitihani.
SOMA HII :Jinsi ya Kuthibitisha Udahili wa Chuo TCU 2025 /2026
Ili kuona majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Chuo cha Maji (Water Institute – WI) kwa mwaka wa masomo 2025, unaweza kufuata hatua zifuatazo:
Majina Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Cha Maji
Kwa mwaka wa masomo2025, Chuo cha Maji (Dar es salaam Water Institute – WI) kimechagua jumla ya wanafunzi 403 kujiunga na programu mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo. Majina ya waliochaguliwa yanaweza kupatikana kupitia tovuti rasmi ya chuo au kupitia kiunganishi kilichopo mwisho mwa chapisho hili. Programu zinazotolewa kwa mwaka huu ni pamoja na:
- Shahada ya Maendeleo ya Jamii katika Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira – Wanafunzi 403 wamechaguliwa kujiunga na programu hii. Programu hii inawaandaa wanafunzi kuwa wataalam wa usambazaji wa maji na usafi wa mazingira katika jamii.
- Shahada ya Uhandisi wa Hydrology – Wanafunzi 23 wamechaguliwa kujiunga. Programu hii inalenga kuandaa wataalam wa hydrology, ambao wataweza kushughulikia masuala ya usimamizi wa maji ya juu na chini ya ardhi.
- Shahada ya Hydrogeology na Uchimbaji Visima – Wanafunzi 26 wamechaguliwa kujiunga. Programu hii ni maalum kwa wale wanaotaka kuwa wataalam wa hydrogeology na kuchimba visima vya maji.
- Shahada ya Uhandisi wa Usafi wa Mazingira – Wanafunzi 41 wamechaguliwa. Programu hii inalenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa kusimamia masuala ya usafi wa mazingira na maji taka.
- Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji – Wanafunzi 236 wamechaguliwa. Hii ni programu inayolenga kutoa wataalam wa rasilimali za maji na umwagiliaji.
Jinsi ya Kuthibitisha Udahili Chuo Cha Maji
Kwa wale waliopata udahili katika zaidi ya chuo kimoja, ni muhimu kuthibitisha udahili wako kwenye chuo kimoja tu.
Uthibitisho huu unaweza kufanyika kwa kutumia namba maalum ya siri ambayo itatumwa kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia namba ya simu au barua pepe uliyoitumia wakati wa kutuma maombi. Ni muhimu kufanya uthibitisho huu kabla ya tarehe 21 Septemba, 2025 ili kuhakikisha nafasi yako haipotei.
Mwongozo kwa Wanafunzi Waliokosa Nafasi
Kwa wale ambao hawakufaulu kupata udahili katika awamu ya kwanza, bado mna nafasi ya kuomba katika awamu ya pili ya udahili. TCU imeeleza kuwa awamu ya pili ya udahili itaanza tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2024. Hii ni fursa nyengine kwa wanafunzi kuomba kujiunga na programu mbalimbali zinazotolewa na vyuo nchini.
Kwa maelezo zaidi, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya Chuo cha Maji (www.waterinstitute.ac.tz) au Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili kupata taarifa za ziada kuhusu udahili wa mwaka huu.