
Mamlaka ya Mapato Tanzania Mapema Mwaka Huu ilitangaza Ajira Mpya kwa Vijana wa kitanzania Wenye Sifa na Vigezo ambapo walipitishwa katika Mchujo wa Interview 2 Written na Oral interview ,Ikiwa ni shauku ya kila aliyefanya Usaili kutaka kujua kama Jina lake limepita kuitwa kazini Hapa tumekuandalia Makala itakayokupa muongozo Jinsi ya kuangalia Jina lako kama Umeitwa Kazini.
Hatua za Kuangalia Majina ya Waliopata Kazi TRA 2025
Tembelea Tovuti Rasmi ya TRA
Fungua tovuti ya TRA kupitia kiungo hiki: www.tra.go.tz.Nenda kwenye Sehemu ya “Taarifa kwa Umma” au “Ajira”
Katika ukurasa wa mwanzo, tafuta sehemu yenye kichwa kama “Taarifa kwa Umma” au “Ajira” ambapo matangazo ya nafasi za kazi na matokeo ya usaili huwekwa.Tafuta Tangazo la Majina ya Waliopata Kazi
Angalia tangazo linalohusiana na majina ya waliopata kazi kwa mwaka 2025. Kwa mfano, unaweza kuona tangazo lenye kichwa kama “MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA” ambalo linaorodhesha majina ya waliochaguliwa.Pakua na Fungua Faili la PDF
Baada ya kupata tangazo husika, pakua faili la PDF lililoambatanishwa na lifungue ili kuona orodha ya majina ya waliopata kazi.Tumia Kipengele cha Utafutaji
Ili kurahisisha utafutaji wa jina lako, tumia kipengele cha utafutaji katika programu ya kusoma PDF kwa kubonyeza “Ctrl + F” kisha andika jina lako kamili au namba ya usaili.Angalia Barua Pepe au Simu
TRA pia inaweza kutuma taarifa moja kwa moja kwa waliofanikiwa kupitia barua pepe au simu. Hivyo, hakikisha unakagua barua pepe yako na ujumbe wa simu mara kwa mara.Wasiliana na TRA kwa Maelezo Zaidi
Ikiwa hukupata taarifa unazohitaji, unaweza kuwasiliana moja kwa moja na TRA kupitia namba ya simu: +255 22 2116453 au tembelea ofisi yao iliyopo:Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
28 Edward Sokoine Drive,
11105 Mchafukoge,
Ilala CBD, S.L.P 11491,
Dar es Salaam, Tanzania.


