Fahamu mchanganuo wa madaraja ya ufaulu kidato cha site (Grading system) kufahamu alama ya ufaulu wako ,Makala hii imechambua alama zote A mpaka F Sambamba na maksi zake.
Alama za Ufaulu Kidato cha Sita
Uchakataji wa matokeo ya Upimaji wa Kidato cha Sita umezingatia viwango vya alama , madaraja ya ufaulu na utaratibu wa matumizi ya alama endelevu (CA) kama ifuatavyo
Gredi | Alama | Uzito Wa Gredi (Pointi) | Maelezo |
A | 80-100 | 1 | Excelent |
B | 70-79 | 2 | Very Good |
C | 60-69 | 3 | Good |
D | 50-59 | 4 | Average |
E | 40-49 | 5 | Satisfactory |
S | 35-39 | 6 | Subsidiary |
F | 0-34 | 7 | Fail |
Madaraja ya ufaulu kidato cha Sita
Mfumo wa madaraja ya ufaulu kwa mtihani wa kidato cha sita unabainishwa kwa kutumia mbinu mbili:
- Jumla ya Alama (Total Point Grading System)
- Divisheni.
Katika mfumo wa Jumla ya Alama, kila somo litakuwa na uzito maalum kulingana na ugumu na umuhimu wake. Alama za mwanafunzi katika kila somo zitazidishwa na uzito wa somo husika, na jumla ya alama hizo zitaamua daraja la mwanafunzi.
Mfumo wa Divisheni unajumuisha kugawa wanafunzi katika makundi (divisions) kulingana na ufaulu wao wa jumla. Kila kundi litawakilisha kiwango fulani cha ufaulu, na wanafunzi watapangwa katika kundi husika kulingana na alama zao. Mbinu hizi mbili hutumika kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa ufaulu wa mwanafunzi unapimwa kwa usahihi na kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.
Watahiniwa waliofanya masomo matatu ya tahasusi au zaidi watapata Daraja la I, II, III, au IV kulingana na jumla ya alama zao.
Watahiniwa waliofanya chini ya masomo matatu ya tahasusi watafaulu kwa daraja la IV ikiwa watafaulu angalau masomo mawili katika Gredi S au somo moja katika Gredi A, B, C, D, au E.
SOMA HII :Jinsi ya kupata passport ya kusafiria na Hati ya Kusafiria
Jedwali lifuatalo linaonesha Madaraja ya ufaulu kidato cha sita yanayotumiwa na baraza la mitihani Tanzania (NECTA)
Daraja | ACSEE (K6) | Maelezo |
I | 3-9 | Bora sana (Excellent) |
II | 10-12 | Vizuri sana (Very Good) |
III | 13-17 | Vizuri (Good) |
IV | 18-19 | Inaridhisha (Satisfactory) |
0 | 20-21 | Feli (Fail) |