Jeshi la Polisi Tanzania kila mwaka Hutangaza Nafasi za kujiunga kulitumikia Jeshi hilo kwa Vijana wa Kitanzania wenye Sifa na Vigezo,Makala hii imekuorodheshea sifa zote unazopaswa kuwa nazo ili kuchaguliwa kujiunga kulitumikia jeshi la polisi.
Vigezo na sifa za kujiunga na jeshi la polisi
Ili kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania mwombaji anatakiwa kutimiza sifa zifuatazo:
- Mwombaji awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 25 kwa waombaji wa kidato cha nne, sita, na astashahada.
- Au kati ya miaka 18 na 30 kwa waombaji wa shahada na stashahada.
- Waombaji wa kidato cha nne wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2023 na wawe na daraja la I hadi IV, wenye daraja la IV wawe na alama 26 hadi 28.
- Waombaji wa kidato cha sita wawe wamehitimu kuanzia mwaka 2018 hadi 2023 na wawe na daraja la I hadi III.
- Waombaji wa astashahada, stashahada, na shahada wawe wamehitimu katika fani zinazohitajika na Jeshi la Polisi.
- Wanaume wawe na urefu usiopungua futi 5 na inchi 8, wanawake wawe na urefu usiopungua futi 5 na inchi 4.
- Mwombaji awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka NIDA.
- Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
- Pia, anatakiwa kuwa na afya njema ya kimwili na kiakili, iliyothibitishwa na daktari wa serikali.
- Aidha, mwombaji anatakiwa awe hajaoa/kuolewa na hana mtoto.
- Ni sharti pia kwamba hajawahi kutumia dawa za kulevya na yuko tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya polisi.
- Mwombaji hapaswi kuwa ameajiriwa na taasisi yoyote ya serikali.
- Zaidi ya hayo, anatakiwa kuwa tayari kufanya kazi za polisi popote nchini Tanzania, kujigharamia katika hatua zote za usaili, asiwe na alama za kuchorwa mwilini, na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
SOMA HII : Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu
Mchakato wa Kutuma Maombi ya Kazi Jeshi la Polisi
Ili kuomba nafasi za kazi kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania, fuata maelekezo yafuatayo hapa chini.
Andika barua ya maombi
Mwombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi kwa mkono wake mwenyewe (handwriting). Katika barua, ni muhimu kuhakikisha kuwa namba za simu za mwombaji zimeandikwa kwa usahihi. Barua hii itumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkuu wa Jeshi la Polisi
S.L.P 961
DODOMA
Omba kupitia mfumo wa mtandaoni
Baada ya kutuma barua ya maombi, mwombaji anatakiwa kuwasilisha maombi yake kupitia mfumo wa ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL). Mfumo huu unapatikana kwenye tovuti rasmi ya Jeshi la Polisi: ajira.tpf.go.tz
Ni muhimu kuzingatia kwamba hatua zote mbili, yaani kutuma barua ya maombi na kuomba kupitia mfumo wa mtandaoni, ni lazima zifuatwe ili maombi ya mwombaji yaweze kuzingatiwa.