Namba ya NIDA (National Identification Number) ni muhimu kwa shughuli nyingi za kiserikali na binafsi, kama vile kufungua akaunti ya benki, kusajili laini ya simu, na kupata huduma za afya. Ikiwa umeshasajiliwa na NIDA lakini hujui namba yako, unaweza kuipata kwa urahisi kupitia simu yako ya mkononi bila kulazimika kwenda ofisi za NIDA. Katika makala hii, tutakuelekeza jinsi ya kupata namba yako ya NIDA kwa haraka kwa kutumia simu.
Hatua za Kufuata lli Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS
Hii ni njia rahisi na ya haraka zaidi ya kupata namba yako ya NIDA. Fuata hatua hizi:
- Fungua sehemu ya ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu yako.
- Andika ujumbe wenye muundo ufuatao:
NIDA#Namba ya Kitambulisho cha Mpiga Kura au Namba ya Simu Uliyosajili NIDA
- Tuma ujumbe huo kwenda 15096.
- Subiri ujumbe wa majibu utakaoonyesha namba yako ya NIDA ikiwa taarifa zako zipo kwenye mfumo wa NIDA.
Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu Kupitia USSD
USSD kwa kirefu (Unstructured Supplementary Service Data)hii ni njia ya kuangalia namba yako ya NIDA kwa kutumia code maatumu za simu. Hii pia ni njia rahisi kwenye kupata namba yako ya NIDA
Hatu za Kupata Namba ya NIDA Kwa USSD
- Piga *152*00# kwenye simu yako ya mkononi.
- Chagua namba 3 (Ajira na Utambuzi).
- Chagua namba 2 (NIDA).
- Ingiza majina yako kamili kama ulivyo jisajili na NIDA mfano, “Alex John Msekwa”
- Kisha ingiza namba ya simu uliyojaza kwenye fomu ya maombi
- Kubali ombi lako.
- Utapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye namba yako ya NIDA.
Masuala Yanayoweza Kujitokeza na Jinsi ya Kuyatatua
Wakati wa kutafuta namba yako ya NIDA, unaweza kukumbana na changamoto zifuatazo:
- SMS haifanyi kazi: Hakikisha umetuma ujumbe kwa namba sahihi (15096) na unatumia namba ya simu sahihi au namba ya kitambulisho cha mpiga kura.
- Hakuna taarifa zinazopatikana: Inawezekana bado hujasajiliwa na NIDA au kuna makosa katika taarifa zako. Katika hali hii, unapaswa kutembelea ofisi za NIDA zilizo karibu.