Form Five Selection 2025 Ruvuma – Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Ruvuma

Form Five Selection 2025 Ruvuma – Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Ruvuma
Form Five Selection 2025 Ruvuma – Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Ruvuma

Hatua kwa Hatua fahamu Jinsi unvyoeza kuangalia Shule za form  five Mkoani Ruvuma na Halmashauri za wilaya zake walizopangiwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2024.

Jinsi ya Kuangalia Selection za Form Five Mkoani Ruvuma

TAMISEMI ndio chombo rasmi kinachosimamia upangaji wa wanafunzi wa kidato cha tano. Kupitia tovuti yao, unaweza kuona shule uliyochaguliwa kwa kutumia jina lako au namba ya mtihani.

Hatua kwa Hatua:

  1. Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
     https://selform.tamisemi.go.tz

  2. Bonyeza sehemu iliyoandikwa “Selection Kidato cha Tano 2025”

  3. Chagua Mkoa – Ruvuma

  4. Teua Halmashauri unayotaka kuangalia

  5. Tafuta jina la mwanafunzi kwa kutumia:

    • Namba ya Mtihani

    • Jina Kamili la Mwanafunzi

Mfumo huu utakuonesha shule aliyopangiwa mwanafunzi, tahasusi (combination), na mahali ilipo shule hiyo.

Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma

Mkoa wa Ruvuma una halmashauri mbalimbali zinazoratibu utoaji wa elimu ya sekondari. Halmashauri hizi ndizo husimamia shughuli zote za shule za sekondari, ikiwemo kupanga wanafunzi na utoaji wa taarifa muhimu kwa wazazi.

Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma:

  1. Songea Municipal Council

  2. Songea District Council

  3. Mbinga Town Council

  4. Mbinga District Council

  5. Nyasa District Council

  6. Tunduru District Council

  7. Namtumbo District Council

 Shule za Advance (Kidato cha Tano) Mkoani Ruvuma

Mkoa wa Ruvuma una shule kadhaa za sekondari zinazotoa masomo ya tahasusi kwa kidato cha tano na sita (A-Level). Baadhi ya shule hizi ni za serikali na zingine binafsi, na zinahudumia wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania.

Baadhi ya Shule Maarufu za Advance Mkoani Ruvuma:

  • Songea Boys High School

  • Songea Girls Secondary School

  • Mbinga Secondary School

  • Tunduru Secondary School

  • Likuyuseka Secondary School

  • Lituhi Secondary School

  • Mtipwili Secondary School

  • Lusewa Secondary School

SOMA HII :  Chuo cha Ualimu Safina Teachers College Online Applications

Kila shule ina mchanganyiko tofauti wa tahasusi kulingana na uwezo wake na idadi ya wanafunzi inayoweza kuhudumia.

 Jinsi ya Kupata Form Five Joining Instruction – Shule za Mkoa wa Ruvuma

Fomu ya kujiunga (Joining Instructions) ni muhimu sana kwa mwanafunzi anayepangiwa shule mpya. Fomu hii ina maelezo ya:

  • Tarehe ya kuripoti

  • Mahitaji ya shule (sare, vifaa vya masomo n.k.)

  • Ada na michango

  • Taratibu za usajili na maelekezo mengine muhimu

Hatua za Kupakua Joining Instruction:

  1. Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
     https://selform.tamisemi.go.tz/Content/selection-and-joining-instructions

  2. Chagua Mkoa – Ruvuma

  3. Chagua Shule aliyopangiwa mwanafunzi

  4. Bonyeza Download kupakua nyaraka hiyo

 Ni muhimu kusoma kwa makini maelekezo yaliyomo kwenye fomu kabla ya mwanafunzi kujiunga shuleni.

About Burhoney 4809 Articles
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati