Wanafunzi au walezi ambao watoto wao walifaulu katika mtihani wa kidato cha nne Sasa wanaweza kuona kama Vijana wao wamepangiwa shule Jijini mwaza? Hapa tumekuwekea hatua zitakazokuwezesha kujua au kuangalia majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Mwanza.
Jinsi ya Kuangalia Selection za Form Five – Jijini Mwanza
Kwa wanafunzi waliopata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano, hatua ya kwanza ni kuangalia orodha ya waliochaguliwa. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hutangaza majina ya wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano kupitia tovuti rasmi.
Hatua za Kuangalia Majina ya Waliopangiwa:
Tembelea tovuti ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tzBonyeza kiungo cha “Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Tano 2025”
Chagua Mkoa – Mwanza au Jiji la Mwanza
Chagua Halmashauri ndani ya jiji la Mwanza, mfano: Nyamagana, Ilemela
Tafuta jina lako kwa kutumia:
Namba ya mtihani au
Shule aliyotoka mwanafunzi
Mfumo huu pia hukuruhusu kuona jina la shule aliyopangiwa mwanafunzi.
Halmashauri za Jijini Mwanza
Jiji la Mwanza linajumuisha halmashauri mbili kuu ambazo zinaratibu shule za sekondari ya juu. Halmashauri hizi ni muhimu kwa wanafunzi waliopangiwa shule ndani ya jiji la Mwanza. Halmashauri hizo ni:
Halmashauri ya Jiji la Nyamagana
Halmashauri ya Jiji la Ilemela
Katika kila halmashauri, kuna shule nyingi za kidato cha tano zinazopokea wanafunzi kila mwaka. Baadhi ya shule maarufu ni:
Mwanza Secondary School
Nyamagana Secondary School
Ilemela Secondary School
Kohovela Secondary School
Mabatini Secondary School
Nanchang Secondary School
Shule hizi ni kati ya zile zinazotumika kutoa elimu bora ya kidato cha tano kwa wanafunzi wa jiji hili.
Jinsi ya Kupata Form Five Joining Instructions – Shule za Jijini Mwanza
Baada ya mwanafunzi kujua shule aliyopangiwa, ni muhimu kupakua fomu ya maelekezo ya kujiunga (Joining Instructions). Fomu hii ina taarifa muhimu kuhusu mambo yote ambayo mwanafunzi atahitaji kabla ya kuripoti kwenye shule aliyo pangiwa.
Hatua za Kupata Fomu ya Joining Instructions:
Nenda kwenye tovuti rasmi ya TAMISEMI:
https://selform.tamisemi.go.tz/Content/selection-and-joining-instructionsChagua Mkoa – Mwanza
Tafuta jina la shule mwanafunzi aliyopangiwa
Bonyeza Download ili kupakua fomu ya maelekezo
Chapisha (print) au hifadhi kwenye kifaa chako cha kielektroniki
Fomu hii ni muhimu kwa mwanafunzi kwani inaeleza vitu vyote muhimu kama tarehe ya kuripoti, vifaa vya shule, michango ya shule, na taratibu za usajili.