Kwa mama Mjamzito Hasa wenye Mimba changa kuna Dalili au ishara Ukiziona wakati wa mimba yako hasa ikiwa changa jua ni hatari zinaweza kuashiria Mimba yako inaharibika au kutoka hivyo Ukiona Dalili Moja ama zote kati ya zifuatazo muone Daktari.
Dalili za Kawaida Ambazo siyo hatarishi
Dalili nyingi kati ya hizi siyo hatari, na haitakiwi kupata hofu sana. Japo unaruhusiwa kumpigia daktari wako na kumuuliza ili upate uhakika zaidi. Dalili nyingi ya hizi zinajitokeza mimba ikiwa changa, na zingine baadae
- kutapika
- kutokwa na uchafu mwingi ukeni
- kichwa kuuma
- uchofu na kizunguzungu
- maumivu yanayokuja kwa haraka na kupotea
- kupungua uzito
- kuhisi joto kali
- kushindwa kuvuta hewa vizuri
- mawazo, na kupata hofu ana kushindwa kufanya kazi zako vizuri
Dalili hizi zinatokea mda wowote wa ujauzito. Japo mimba inapokuwa changa zaidi ndipo hatari ya mimba kuharibika inakuwa kubwa, ila watakiwa kuwa makini kipindi chote.
1. DAMU UKENI
hata kama utaona spotting/vitone vidogo vya damu usikubali mtu akwambie ni kawaida jinyanye nenda hospital mapema ukafanyiwe vipimo
2. KUVIMBA MWILI MZIMA
hii mara nyingi husababishwa na presha kuwa juu mama anaweza kuvimba miguu sana na uso na mikono pia. Ukiona hii dalili wahi hospital
3.MAUMIVU YA TUMBO
Kuna yale maumivu ya kawaida yanayosababishwa na uterus kutanuka hasa kuanzia 2nd trimester haya hayana shida ila kuna maumivu makali sana ambayo hayavumiliki, ukipata hayo wahi mapema
4. KUACHA KUONA, KICHWA KUUMA KULIKO KAWAIDA
Hizi zinaweza kuwa dalili za presha na sukari ya mwili kutokuwa sawa ni muhimu kuhakikisha unafika hospital kupata msaada
5. HOMA KALI NA DEGEDEGE
6. CHUPA KUPASUKA KABLA YA UCHUNGU
Hata kama imefika week zako za kujifungua ukiona chupa imepasuka maji yanatoka ukeni kwa mfululizo na huna dalili za uchungu wahi mapema hospital usianze kusubiri uchungu uanze
7. MAJI KUTOKA UKENI
Wapo ambao hupata hii hali mapema njia inaweza kuwa inafunguka kutokana na kazi nzito hivyo mama anapata leakage maji kutoka kidogo kidogo ni vyema kwenda ufanyiwe uchunguzi isijepelekea maji yakapungua au kuisha kwa mtoto na wakati muda wa kuzaliwa bado.
8.Kutapika na kichefuchefu kupita kiasi
Kwa mjamzito ni kawaida kupata kichefuchefu, lakini kama tatizo ni kubwa inaweza kuashiria shida kubwa ya kiafya. Kama unashindwa mpaka kula au kunywa chochote, hapo utaishiwa maji. Na kuishiwa maji inaweza kuhatarisha ujauzito wako.
Kama unahisi kizunguzungu kinakutesa sana, ongea na daktari atakupa dawa ya kupunguza makali yake.
9.Mtoto kuacha kucheza
Mtoto kupunguza kucheza inaweza kuashiria kachoka, hii ni kawaida isikupe hofu. ila kama hachezi kabisa kwa siku nzima, hapo kuna shida kubwa.
Sasa ili kugundua tatizo, inashauriwa ukiona mtoto hachezi mda mefu, jaribu unywe kitu cha baridi. Kisha lala kwa ubavu, na fatilia kama mtoto ataanza kucheza.
Mpigie daktari, ama nenda hospital haraka endapo utagundua mtoto ameacha kucheza. Daktari atafanya vipimo kuona kama kuna hatari yoyote.
10.Kupata uchungu mapema mimba ya miezi 7
Kupata uchungu na mimba haijatimiza umri wa kujifungua, ni dalili mbaya. Kama tumbo linavuta na kuachia na hii hali itokee mara chache na kuisha hilo ni kawaida. Kwani hata ukifika kileleni baada ya tendo, lazima utahisi tumbo kuvuta.
11.Chupa kupasuka mapema ni dalili mbaya kwa mjamzito
Tunaposema chupa, tunamaanisha ule mfuko unaobeba mtoto. Mfuko huu unakuwa na maji yanayomlinda mtoto asiumie. Mfuko unapasuka pale mama akianza uchungu na yupo tayari kujifungua. Endapo mfuko utapasuka mapema na mtoto akaendelea kubaki tumboni, mtoto atakosa hewa na kupoteza uhai.
12.Maumivu makali yasiyoisha kwenye kichwa, tumbo na kushindwa kuona vizuri
Hizi dalili zinaweza kuashiri kupanda kwa presha kitaalamu (preeclampsia) . Hili ni tatizo baya na linaweza kupelekea kifafa cha mimba. Tatizo linaambatana na dalili za presha kupanda na protini nyingi kwenye mkojo, hasa inatokea baada ya week 20 za ujauzito. Hakikisha unaenda hospital haraka endapo unahisi dalili hizo.