Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ni tatizo linalowapata watu wa jinsia zote na umri wote. Maumivu haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na mara nyingi husababishwa na matatizo katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mfumo wa uzazi, au njia ya mkojo.
Nini kinapelekea maumivu ya Tumbo chini ya kitovu?
Maumivu haya yanaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, ikiwemo matatizo ya kiafya yanayoathiri viungo vilivyo eneo hilo kama vile utumbo, kibofu cha mkojo, na via vya uzazi kwa wanawake. Zifuatazo ni baadhi ya sababu kuu:
Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI)
Hii ni mojawapo ya sababu za kawaida za maumivu chini ya kitovu, hasa kwa wanawake. Maambukizi haya hutokea pale bakteria wanapoingia kwenye kibofu cha mkojo na kusababisha muwasho na maumivu.
Dalili:
Maumivu wakati wa kukojoa
Kukojoa mara kwa mara lakini kiasi kidogo
Mkojo wenye harufu mbaya au wenye rangi isiyo ya kawaida
Homa na kuhisi baridi
Tiba:
Kutumia dawa za antibiotiki baada ya ushauri wa daktari
Kunywa maji mengi kusaidia kusafisha kibofu
Kuepuka kushikilia mkojo kwa muda mrefu
Matatizo ya Uzazi kwa Wanawake
Wanawake wanaweza kupata maumivu chini ya kitovu kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi kama vile:
Hedhi (Menstrual Cramps)
Maumivu haya hutokea wakati wa hedhi kutokana na mikazo ya mfuko wa uzazi.
Husababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu na mgongo wa chini.
Endometriosis
Hali hii hutokea pale ambapo tishu zinazofanana na zile za ndani ya mfuko wa uzazi hukua nje ya mfuko wa uzazi.
Hii husababisha maumivu sugu, hasa wakati wa hedhi au tendo la ndoa.
Mimba Isiyo Kwenye Mfuko wa Uzazi (Ectopic Pregnancy)
Hii hutokea pale ambapo yai lililorutubishwa linajikita nje ya mfuko wa uzazi, mara nyingi kwenye mirija ya fallopian.
Husababisha maumivu makali upande mmoja wa tumbo chini ya kitovu na inaweza kuwa hatari kwa maisha.
Tiba:
Matibabu hutegemea chanzo, ikiwa ni hedhi ya kawaida, unaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu kama ibuprofen.
Kwa endometriosis na matatizo mengine, daktari anaweza kupendekeza matibabu ya homoni au upasuaji.
Soma hii :Sababu Kwanini mwanamke anapata maumivu wakati wa tendo na Tiba yake
Matatizo ya Mfumo wa Mmeng’enyo wa Chakula
Kuharisha au Kufunga Choo (Constipation)
Choo kigumu au kinachoshindikana kutoka kinaweza kusababisha maumivu chini ya kitovu.
Hii mara nyingi husababishwa na ulaji wa chakula kisicho na nyuzinyuzi, upungufu wa maji mwilini, au kutofanya mazoezi.
Saratani ya Utumbo Mpana (Colon Cancer)
Ingawa si sababu ya kawaida, saratani ya utumbo inaweza kusababisha maumivu sugu, kupungua uzito bila sababu, na kubadilika kwa mpangilio wa haja kubwa.
Tiba:
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi kama mboga za majani na matunda.
Kunywa maji mengi ili kuzuia kufunga choo.
Kutumia dawa za kulainisha choo ikiwa inahitajika.
Appendicitis (Kuuma kwa Utumbo Mfu – Appendiksi)
Hili ni tatizo la dharura linalotokea pale ambapo kiungo kinachoitwa appendix kinapovimba na kujaa usaha.
Husababisha maumivu makali chini ya kitovu, hasa upande wa kulia, na yanaweza kuongezeka kwa muda.
Dalili:
Maumivu makali upande wa kulia chini ya kitovu
Homa na kichefuchefu
Kupoteza hamu ya kula
Tiba:
Appendicitis huhitaji matibabu ya haraka na mara nyingi upasuaji wa kuondoa kiungo hicho.
Mawe kwenye Figo (Kidney Stones)
Mawe kwenye figo yanaweza kusababisha maumivu makali chini ya kitovu, hasa yakisafiri kuelekea kibofu cha mkojo.
Dalili:
Maumivu makali upande wa mgongo au chini ya kitovu
Damu kwenye mkojo
Kichefuchefu na kutapika
Tiba:
Kunywa maji mengi kusaidia kusukuma mawe madogo kutoka kwenye figo.
Dawa za kutuliza maumivu.
Upasuaji ikiwa mawe ni makubwa na hayawezi kutoka yenyewe.
Tiba za Jumla za Maumivu Chini ya Kitovu
Matibabu ya maumivu haya hutegemea chanzo chake, lakini kuna njia za jumla za kusaidia kupunguza maumivu:
Kutumia Dawa za Kupunguza Maumivu
Dawa kama paracetamol au ibuprofen zinaweza kusaidia kupunguza maumivu yanayosababishwa na hedhi, maambukizi madogo, au matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.
Kunywa Maji Mengi
Maji husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na huzuia mawe ya figo na tatizo la kufunga choo.
Lishe Bora
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi kama mboga, matunda, na nafaka.
Epuka vyakula vyenye mafuta mengi na vyakula vya kusindika ambavyo vinaweza kusababisha gesi na matatizo ya utumbo.
Kupumzika na Kufanya Mazoezi
Mazoezi husaidia kuimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kupunguza msongo wa mawazo unaoweza kuongeza maumivu.
Kupata Ushauri wa Daktari
Ikiwa maumivu yanakuwa makali, yanaendelea kwa muda mrefu, au yanaambatana na dalili zingine kama homa, kichefuchefu, au damu kwenye kinyesi/mkojo, ni muhimu kumuona daktari.
Je maumivu ya tumbo chini ya kitovu ni tatizo kubwa?
Kama tulivoona hapo juu, maumivu ni kiashiria kwamba kuna tatizo fulani la kiafya kwenye mwili. Ni ngumu kutambua chanzo kwa kufatilia maumivu pekee. Ni muhimu kumwona daktari akupime kugundua chanzo cha tatizo. Daktari atakupa dawa za kupunguza maumivu wakati huo atashugulika kujua chanzo.
Nini chanzo kikubwa cha maumivu ya tumbo chini ya kitovu?
Viungo kama utumbo mkubwa na mdogo vipo eneo la tumbo la chini, na vinachukua nafasi kubwa sana pale. Kwa sababu hiyo changamoto yoyote inayoathiri utumbo basi yaweza kuwa chanzo cha maumivu chini ya kitovu.
Changamoto hizi za kila siku ni pamoja na
- gesi tumboni
- chakula kutosagwa vizuri
- kuharisha na
- kukosa choo na choo kigumu
Kama chakula hakisagwi vizuri na tumbo kujaa, waweza kuwa na aleji na aina fulani ya chakula, ama tumbo lako haliwezi kusaga aina fulani cha chakula. Suluhisho ni kuacha kabisa kutumia aina ya chakula ambacho unaona mwili umekikataa.
Pia yawezekana utumbo umebimba kwa ndani. Magonjwa yanayopelekea utumbo kuvimba ni pamoja na
- vudonda vya tumbo
- maambukizi ya bakteria
- Celiac disease (ambapo mwili unashambulia kiambata cha guleten ambacho hupatikana kwenye ngano)
- Majeraha kwenye utumbo mdogo na mpana na
- Saratani kwenye utumbo
Je nini chanzo cha maumivu ya tumbo kwa mwanamke?
Kama wewe ni mwanamke, viungo vya uzazi vipo eneo la chini ya kitovu. Viungo hivi ni chanzo kingine kikubwa cha maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Japo maumivu ya tumbo la hedhi ni kawaida kwa kila mwanamke, sometime yanaweza kuashiria uwepo wa changamoto flani ya kiafya kama
- PID
- Vimbe kwenye kizazi (fibroids)
- Kizazi kututumka (endometriosis)
- Saratani ya kizazi
- Vimbe kwenye mayai
Magonjwa ya Figo
Kama tatizo siyo kwenye mfumo wa chakula, basi yawezekana kuna shida kwenye njia ya mkojo ambako figo zinahusika. Ugonjwa mkubwa kwenye njia ya mkojo ni UTI yani maambukizi ya bakteria kwenye njia ya mkojo. UTI inaweza kuathiri kibofu cha mojo, mirija ya kusafirisha mkojo na hata figo pia. Na matatizo yote haya huzalisha maumivu kwenye kitovu.
Vipi kama maumivu ya tumbo yanatokea upande wa kushoto au kulia?
Maumivu ya tumbo upande wa kushoto chini ya kitovu yanaweza kutokana na athari kwenye utumbo mpana. Yawezekana kukawa na bakteria waliojificha eneo hilo na kupelekea kututumka mpaka kuleta maumivu.
Maumivu yakiwa eneo la chini kulia, yaweza kuwa ni appendix. Hiki ni kifuko kidogo ambacho huhifadhi mawe. Kifuko kinaweza kushambuliwa na bakteria ama kikajaa uchafu na hivo suluhishi ikawa ni kukiondoa kabisa.
Pia Maumivu kulia na kushoto kwa chini inaweza kutokana na athari kwenye mifuko ya mayai ama figo. Uvimbe kwenye yaia au mawez kwenye figo vyote hupelekea upate maumivu. Pia kama yai linatolewa kwenye kikonyo siku ya hatari, laweza kupelekea maumivu haya.