Kipimo cha mimba ni moja ya njia bora za kubaini ikiwa mwanamke ni mjamzito au la. Kipimo hiki kinachunguza uwepo wa homoni ya hCG (Human Chorionic Gonadotropin) ambayo huzalishwa baada ya yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba. Hii ni homoni inayozalishwa mapema baada ya kutungika kwa mimba, na inaweza kupimwa kupitia mkojo au damu.
Kipimo cha Mimba ni nini?
Kipimo cha ujauzito wa nyumbani (HPT) ni kipimo kinachothibitisha ujauzito nyumbani. Ni kipimo cha bei nafuu kinachotumia sampuli ya mkojo wako na kutafuta homoni maalum ya ujauzito; gonadotropini ya chorionic ya binadamu (hCG). Uzalishaji wa HCG huanza mara tu kiinitete kinapopandikizwa kwenye uterasi.
Kuna njia mbili za kuthibitisha ujauzito; seti ya ujauzito nyumbani na mtihani wa damu. Vipimo vyote viwili hutafuta homoni ya hCG katika mwili kupitia mkojo au damu.
Kwa mtihani wa ujauzito wa nyumbani, ishara ya mstari mmoja au mbili nyekundu inathibitisha mimba.
Aina za Kipimo cha Mimba
Kipimo cha Mkojo (Pregnancy Test Kit): Kipimo hiki ni rahisi na kinapatikana kwenye maduka ya dawa na hutumika nyumbani. Kila kipimo cha mkojo kina maelekezo yake, lakini kwa kawaida huchukua dakika chache ili kupata majibu. Kipimo hiki kinapima kiwango cha hCG kilichopo kwenye mkojo.
Kipimo cha Damu (Blood Test): Huu ni kipimo kinachofanyika hospitalini na kinachangia kugundua ujauzito mapema zaidi kuliko kipimo cha mkojo. Kipimo hiki kinapatikana kwa aina mbili:
Kipimo cha hCG cha jumla: Kinagundua uwepo wa homoni ya hCG kwenye damu.
Kipimo cha hCG cha kiasi: Hupima kiwango cha homoni ya hCG kwenye damu, na kinaweza kutumika kugundua ujauzito mapema zaidi.
Soma Hii :Madhara ya kutofanya mapenzi muda mrefu kwa mwanaume
Maandalizi ya kufanya kipimo cha mimba cha mkojo
Kama unafanya kipimo ukiwa nyumbani, hakikisha unazingatia yafuatayo
- unasoma kwa uangalifu maelekezo ya matumizi, kwenye pakiti lenye kifaa cha kupimia kabla hujaanda mkojo wa kupima
- kipimo hakijaexpire
- pima mkojo wa kwanza wa asubuhi baada ya kupitisha hedhi yako
- usinywe maji au kinywaji chochote kwa wingi, kwasababu itafanya homoni ya HCG kuwa kidogo na kutoonekana kwenye kipimo.
Jinsi ya Kufanya Kipimo cha Mimba Nyumbani
Pata pregnancy test kit kutoka kwenye duka la dawa au hospitali.
Kusanya mkojo wa asubuhi, kwani huu huwa na kiwango cha juu cha hCG.
Mimina kiasi kidogo cha mkojo kwenye sehemu ya kupimia au tumia kijiti cha kipimo kulowesha mkojo moja kwa moja.
Subiri kwa muda uliopendekezwa kwenye maelekezo ya kipimo, mara nyingi ni kati ya dakika 3-5.
Soma matokeo kulingana na mistari inayojitokeza kwenye kipimo.
Jinsi ya Kusoma Majibu ya Kipimo cha Mimba
Mstari mmoja (–) wa kudhibiti pekee:
Hii inamaanisha hakuna ujauzito. Kipimo hakikudhibitisha uwepo wa homoni ya hCG kwenye mkojo.Mistari miwili (++):
Ikiwa mstari wa kudhibiti na mstari mwingine wa pili vinajitokeza, hii inamaanisha ujauzito upo. Hata hivyo, mstari wa pili unaweza kuwa hafifu, lakini bado inadhihirisha kuwa kuna ujauzito.Hakuna mstari wowote:
Ikiwa hakuna mstari wowote unaojitokeza, kipimo hakikufanya kazi na inashauriwa kurudia tena kipimo au kutumia kipimo kingine.
Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Kufanya Kipimo
Hakikisha kipimo hakijapita muda wake wa matumizi.
Soma maelekezo ya kipimo kwa umakini.
Ikiwa matokeo ni hasi lakini unahisi dalili za ujauzito, subiri siku chache na jaribu tena.
Ikiwa matokeo ni chanya, ni muhimu kushauriana na daktari kwa uthibitisho zaidi na ushauri wa kiafya.
Nina wasiwasi na majibu nifanyeje?
Endapo hujaridhika na majibu yako, subiri tena wikik moja kisha upime kwa usahihi kama ulivoelekezwa na mtoa huduma alieyekuuzia kifaa. Pia unaweza kwena hospitali na kufanya kipimo cha damu. Kipimo cha damu kinaweza kugundua mimba hata ndani ya wiki moja tu.
Kipimo cha Mimba ni sahihi Kwa asilimia Ngapi?
Maarufu kama UPT kipimo hiki waweza kufanya ukiwa nyumbani kinaweza kukupa usahihi wa matokeo kwa ailimia 99, kama utafuata maelekezo vizuri ya upimaji.
Kipimo cha damu ni sahihi zaidi ya asilimia 99. Kumbuka usahihi wa kipimo kama umejipima mwenyewe nyumbani unategemea jinsi gani umefuata maelekezo ya kupima na umri wa ujauzito
Lini Unatakiwa Kufanya Kipimo cha Mimba?
Baadhi ya vipimo vya homoni ya HCG vinaweza kutoa matokeo hata kabla ya kukosa hedhi yaani week moja baada ya kushika mimba, lakini fahamu kwamba matokeo yatakuwa sahihi zaidi endapo utasubiri wiki moja baada ya kukosa hedhi inayofuata.