Airtel inatoa huduma ya kukopa salio ambapo mteja anaweza kukopa salio la ziada na kulipa baadaye. Hii ni huduma inayowezesha wateja wa Airtel kukopa salio wakati salio lao halitoshi na kisha kulipa unapoongezeka kwa salio lako. Huduma hii ni rahisi kutumia na inapatikana kwa wateja wote wa Airtel wanaotumia simu za mkononi.
Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
Kukopa Salipo Airtel Piga h *149*44#
Vigezo Na Masharti Ya Huduma Ya Airtel Daka Salio
- Huduma hii kitakuwa kinapatikana kwa wateja wa malipo ya kabla
- Huduma hii iitakuwa inapatikana kupitia *149*44 # menyu ya huduma.
- Mtumiaji lazima awe kwenye mtandao wa Airtel kwa angalau siku 90.
- Mtumiaji atalipa ada ya huduma ya 15% kwa ajili ya huduma ya mkopo.
- Ada ya huduma ya 15% inakusanywa wakati wa kuongeza salio.
- Mtumiaji ataomba mkopo, atapokea muda wa maongezi au kifurushi cha kiasi kilichoombwa.
- Mchakato wa ulipaji wa mkopo hutokea wakati mtumiaji anaongeza muda wa maongezi ambapo kiasi cha mkopo kitaondolewa kwanza na salio lilibaki litawekwa katika akaunti kuu ya mtumiaji.
- Mkopo lazima kulipwa baada ya siku 7.
- Airtel haitofidia kwa huduma yoyote iliyonunuliwa. Vifurushi vyote vilivyonunuliwa lazima vitumike kama ilivyoekezwa katika menyu ya huduma.
- Airtel Tanzania PLC ina haki ya kusahihisha au kurekebisha vigezo hivi na masharti au kuondoa bidhaa wakati wowote. Tukio lolote katika hayo, taarifa itakuwa na ufanisi mara moja au kama tarehe ilivyotajwa katika arifu kama hizo.
SOMA HII : Orodha ya Code Za Mitandao ya Simu Tanzania
Faida za Huduma ya Kukopa Salio Airtel
Inasaidia Wakati wa Dharura: Huduma hii ni muhimu sana kwa wateja wanaohitaji kufanya mawasiliano lakini hawana salio la kutosha. Wakati wa dharura, unaweza kukopa salio na kuendelea kutumia huduma za Airtel bila shida.
Inafaa kwa Watumiaji wa Data: Wateja wengi hutumia data kwa biashara, masomo, au mawasiliano ya kila siku. Huduma ya kukopa salio inawawezesha kutumia data hata wanapokuwa na salio la chini.
Rahisi Kutumia: Huduma ya kukopa salio ni rahisi kufikia kwa kupiga *148# na kuchagua “Kopa Salio”. Hakuna haja ya kufuata mchakato mrefu au wa kiufundi.