Close Menu
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
BOFYA HAPA
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home » Mfahamu Brian Deacon Aliyecheza movie ya yesu
Dini

Mfahamu Brian Deacon Aliyecheza movie ya yesu

MFAHAMU Brian Deacon MUIGIZAJI MAARUFU ZAIDI DUNIANI ALIEGIZA KAMA YESU KATIKA MOVIE YA JESUS CHRIST 1979
BurhoneyBy BurhoneyMarch 23, 2025Updated:March 23, 2025No Comments6 Mins Read
Share Facebook Twitter Telegram WhatsApp
Mfahamu Brian Deacon Aliyecheza movie ya yesu
Mfahamu Brian Deacon Aliyecheza movie ya yesu
Share
Facebook Twitter Telegram WhatsApp
JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

Katika ulimwengu wa filamu za kidini, jina la Brian Deacon linahusiana moja kwa moja na taswira ya Yesu Kristo kutokana na uhusika wake katika filamu ya Jesus ya mwaka 1979. Filamu hii imekuwa moja ya filamu za kidini zilizoangaliwa zaidi ulimwenguni na imewafikia mamilioni ya watu katika lugha zaidi ya 1,800. Lakini, Brian Deacon ni nani? Na ni vipi alijikuta katika nafasi hii muhimu?

Maisha ya Awali na Kazi ya Uigizaji

Brian Deacon alizaliwa mnamo tarehe 13 Februari 1949 huko Oxford, Uingereza. Kabla ya kuchukua nafasi ya Yesu katika filamu ya Jesus, Deacon alikuwa tayari ameanza kujijengea jina katika tasnia ya filamu na televisheni. Alishiriki katika filamu na michezo ya kuigiza za Uingereza, lakini nafasi yake kama Yesu ilikuja kuwa kilele cha kazi yake na kubadilisha mkondo wa maisha yake.

Kuteuliwa kwa Nafasi ya Yesu

Kuteuliwa kwa Nafasi ya Yesu

Wakati wa mchakato wa kutafuta mwigizaji wa kumcheza Yesu, waandaaji wa filamu hii walitaka mtu ambaye angeweza kuwakilisha sura ya upole na huruma ya Kristo. Baada ya majaribio mengi, Brian Deacon alichaguliwa, hata ingawa hakuwa mwigizaji mashuhuri kimataifa wakati huo. Iliripotiwa kuwa Deacon alihitaji kung’oa meno yake ya nyuma ili kusaidia kuleta mwonekano sahihi kwa mhusika wake.

Brian Deacon alifanikiwa kupenya katika kundi la waigizaji 1000 waliohojiwa na kubaki 260 waliojaribiwa kwa kuigiza akiwa pekee mwingireza na waliosalia ni wa Israel akapenya hadi kuipata nafasi

Kabla ya kuanza kurekodiwa kwa filamu Brian Deocan alisoma kitabu cha Mtakatifu Luka mara 20 kwa kuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka katika kitabu hicho

Filamu ilirekodiwa takribani miezi 18 na kuna baadhi ya hatari zilitokea ikiwa ni pamoja na hoteli waliyoweka kambi mjini Tel Aiv kushika moto lakini walipona

Tukio lile walilichukulia kama nguvu ya Mungu imewaponya

Brian Deacon ndani ya filamu ya ”JESUS”

Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''

Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

Soma Hii : Filamu ya yesu ilitoka mwaka gani

Changamoto Katika Uigizaji

Kufanya filamu ya Jesus hakukuwa kazi rahisi kwa Brian Deacon na timu yake. Filamu ilirekodiwa katika maeneo halisi ya Mashariki ya Kati, ikiwakilisha mazingira ya kihistoria ya nyakati za Yesu. Deacon alikumbana na changamoto za hali ya hewa, vumbi, na hata changamoto za kiafya wakati wa upigaji picha. Licha ya yote hayo, aliweza kuleta uhai katika uhusika wake na kutoa taswira ya Yesu ambayo imegusa mioyo ya watu wengi.

Athari za Filamu ya Jesus

Athari za Filamu ya Jesus

Filamu ya Jesus imekuwa moja ya filamu zilizo na ushawishi mkubwa katika historia ya sinema za kidini. Tangu ilipozinduliwa mwaka 1979, filamu hii imetafsiriwa katika lugha nyingi zaidi ya filamu nyingine yoyote duniani. Imekuwa nyenzo kuu ya uinjilisti na imeonyeshwa katika sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo hayana ufikiaji rahisi wa maandiko matakatifu.

Maisha Baada ya Filamu

Baada ya kucheza kama Yesu, Brian Deacon aliendelea na kazi yake ya uigizaji, ingawa hakupata tena nafasi kubwa kama hiyo. Aliendelea kushiriki katika filamu na michezo ya televisheni, lakini wengi bado wanamkumbuka kwa jukumu lake katika Jesus. Kwa wengi, sura yake imesalia kuwa taswira ya Yesu kwa vizazi kadhaa.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

Watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.

Watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.

Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.

Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

Maisha ya Brian Deacon Ndoa

Brian alifunga ndoa ya kwanza 1977 na Rula Lesnka hadi kufikia mwaka 1987 ndoa yake ilivunjika walipata mtoto mmoja Lala Decon
1998 alimuoa Natalie Bloch ambaye wapo nae mpaka sasa

Filamu zingine alizowahi igiza Brian Deacon

A zed & Two Noughts 1985, The Feathered serpent 1976-1978 Tamthilia ya Lilie 1978 akiitwa Frank Mile.

JIUNGE NASI WHATSAPP BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA
Follow on Telegram Follow on WhatsApp
Share. Facebook Twitter Email Telegram WhatsApp
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Related Posts

Nyota ya Majina yanayoanzia Herufi G :Tabia zao,Ndoa na Mafanikio

June 16, 2025

Nyota za Majina yanayoanzia Herufi F :Bahati ,Ndoa,Mafanikio na Mapenzi

June 16, 2025

Nyota za Majina yanayoanzia Herufi E :Bahati ,Ndoa,Mafanikio na Mapenzi

June 16, 2025

Nyota za Majina yanayoanzia Herufi D :Bahati ,Ndoa,Mafanikio na Mapenzi

June 16, 2025

Nyota za Majina yanayoanzia Herufi C :Bahati ,Ndoa,Mafanikio na Mapenzi

June 16, 2025

Nyota za Majina yanayoanzia Herufi B : Bahati ,Ndoa,Mafanikio na Mapenzi

June 15, 2025
Leave A Reply Cancel Reply

Latest Posts

Nafasi 137 za Kazi Kutoka UTUMISHI – Taasisi Mbalimbali Juni 2025

June 13, 2025

Nafasi 83 za Kazi Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) June 2025

June 12, 2025

Nafasi za Kazi – NARCO (Kampuni ya Ranchi za Taifa) – Juni 2025

June 12, 2025

Majina ya Walioitwa kazini Ajira Portal Utumishi PSRS 2025 PDF Download

June 12, 2025

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI na Ajira Portal 2025

June 12, 2025
Load More

Subscribe to Updates

Usipitwe na Habari zetu za kila siku Kuwa wa kwanza kupata Habari zetu Kwa Kuandika Email yao Hapo chini

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

swahiliforums.com
Facebook X (Twitter) Instagram WhatsApp Telegram Pinterest
Copyrights reserved @2025 swahiliforum.com

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.