kawaida mimba ya binadamu inatakiwa ibebwe kwa wiki 37 mpaka 42 TU, mwanamke anayezidisha wiki ya 42 bila kuzaa tunaita kitaalamu kama post term pregnancy yaani mimba imepitiliza muda halali wa kuzaliwa.
Sababu za mimba Kupitiliza Muda wake ni nini?
kuhesabu tarehe vibaya; watu wengi wenye matatizo haya hua na historia ya kuhesabu siku zao vibaya na kutoa taarifa ambazo sio sahihi clinic.
utakuta mimba iko kawaida tu na muda wake lakini kwasababu mama alitoa tarehe ambayo sio ya kweli basi anaonekana mimba yake imechelewa.
tatizo ya kurithi; baadhi ya familia ni kawaida kwa vizazi vyote kujikuta vinakua na mimba za kupitiliza hivyo ukiona mimba yako ukiona imepitiliza ni vizuri ukaulizia kwa wazazi na ndugu zako kama hicho kitu hua kinatokea mara kwa mara kwenye ukoo husika.
mimba nje ya kizazi; mimba chache sana hutungwa nje ya kizazi na kukua mpaka kua kubwa kabisa, lakini mimba hizi haziwez kuzaliwa kwa kawaida kwasababu mtoto anakua eneo ambalo haliwezi kupata uchungu hasa kwenye eneo la tumbo la chakula kitaalamu kama abdominal cavity, sasa mimba ya aina hii huweza kuzaliwa kwa upasuaji tu.
mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba ikachelewa kuzaliwa ni unene wa mama mjamzito, mtoto wa kiume tumboni na mimba ya kwanza.
Unaweza kujua umri wa Mimba yako na Tarehe ya Matarajio kwa njia mbalimbali mfano:
- Kutumia Hedhi ya mwisho kabla ya kupata Mimba/Ujauzito.
- Kuhesa kutokea kipindi ambacho Mjamzito anaanza kusikia Mtoto anaanza kucheza Tumboni mwa Mjamzito.
- Kutumia ultrasound ya mwanzoni mwa Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito na nk.
Sababu nyingine zinazoweza kupelekea Mjamzito kuchelewa kujifungua hazijulikana au bado hazijafahamika, Isipokuwa kuna mambo ambayo yanaweza kuhatarisha Mjamzito kuchelewa kujifungua.
Soma Hii :Dalili za Mwanzoni za Kujifungua au Uchungu kwa Mjamzito.
Vihatarishi vinavyopelekea Mjamzito kuchelewa kujifungua ni kama;
- Mimba ya kwanza au Mjamzito anayebeba Ujauzito kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
- Mimba au Mjamzito ambaye amebeba Mtoto jinsia ya Kiume Tumboniumboni.
- Mjamzito ambaye mimba ya kwanza alichelewa kujifungua huweza kuchelewa kujifungua Mimba ya pili kwa 27% au Mimba ya tatu kwa 39%.
- Mjamzito mwenye Uzito mkubwa wa kupindukia BMI ya 30Kg/M² au zaidi.
- Mjamzito ambaye wakati kuzaliwa yeye mwenyewe alichelewa kuzaliwa pia huweza kuchelewa kujifungua.
- Mjamzito anaweza kurithi kuchelewa kujifungua kutoka kwa wazazi wake au kizazi kingine.