Close Menu
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
  • Home
  • Ajira Mpya
  • Elimu
  • Michezo
  • Makala
Facebook X (Twitter) Instagram
swahiliforums.com
Home»Afya»Style za kufanya mapenzi wakati wa ujauzito
Afya

Style za kufanya mapenzi wakati wa ujauzito

Staili Nzuri za Kufanya Tendo la Ndoa Wakati wa Ujauzito ,Mikao ya Kufanya Mapenzi kwa Mjamzito ambayo ni salama
BurhoneyBy BurhoneyMarch 25, 2025Updated:March 25, 2025No Comments4 Mins Read
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Style za kufanya mapenzi wakati wa ujauzito
Style za kufanya mapenzi wakati wa ujauzito
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Ifahamike kwamba, mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa muda wote wa kipindi chake Cha ujauzito.
Hatoshauriwa au kuruhusiwa kushiriki tendo la ndoa Kama ujauzito wake unachangamoto Kama vile MIMBA kutishia kutoka, anaumwa, ameshonwa mlango wa kizazi, anatokwa na damu n.k.

Mitindo ya ufanyaji tendo la ndoa wakati wa ujauzito, hubadilika kadri MIMBA inavyokuwa kubwa.

Mitindo Bora zaidi Ni ile ambayo haitochosha Wala kuleta maumivu, vyema zaidi utumike mtindo wa ubavu ubavu, mwanamke kukaa kwa juu au dog staili.

Mjamzito anapaswa kuepuka mitindo ambayo itampa maumivu ya tumbo au kumchosha zaidi. Aepuke mtindo utakao mfanya alalie mgongo kwa muda mrefu, staili ya kulalia mgongo “kifo Cha mende” kinaweza msababishia mjamzito ashindwe kupumua vizuri na kumletea shida au staili ya kulalia tumbo inaweza mkandamiza mtoto na kumsabishia matatizo.

Ikumbukwe sio kila mwanamke atakuwa na Hamu ya kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito wake hivyo asilazimishwe kufanya hivyo Kama hayuko ridhaa.

Soma hii :Njia rahisi ya Kuitambua Siku ya Kubeba mimba

Je Kufanya Tendo la Ndoa Wakati wa Ujamzito Ni Salama?

Jibu ni ndio, kufanya tendo wakati wa ujauzito ni salama kabisa. Uume kuingia ndani ya uke,zile pilika za kuingiza na kutoa haziwezi kuathiri mtoto, kwa sababu analindwa na tumbo na misuli ya ukuta wa kizazi pia.

Lakini pia mtoto analindwa na majimaji mazito(amniotic fluid).
Usijali kuhusu kusinyaa na kutanuka kwa uke pale unapofikia kilele, hakuwezi kufanya mimba ikatoka. Kutanuka huku ni tofauti na wakati wa kuzaa.

Mazingira gani inashauriwa usifanye tendo la ndoa wakati wa ujauzito?

Daktari anaweza kushauri usifanye tendo la ndoa kama

  • una historia ya mimba kuharibika mara kwa mara
  • uko kwenye hatari ya kupata uchungu mapema kabla ya week 37 za ujauzito
  • unatokwa na damu na maumivu yasijulikana sababu yake
  • chupa imepasuka na maji yanavuja
  • mlango wa kizazi umefunguka mapema zaidi
  • una tatizo kitaalamu placenta previa yani tishu za mirija unaomlisha mtoto chakula na hewa safi, umekuwa mpaka kuziba mlango wa kizazi
  • kama unatarajia kujifungua watoto mapacha

Staili Salama za Kufanya Mapenzi Wakati wa Ujauzito

Mwanamke Ameketi :

Mwanamke anaweza kuketi juu ya mumewe, hii inamruhusu kudhibiti kina na kasi.Hii ni staili nzuri kwa sababu inampa mwanamke udhibiti zaidi juu ya kina na jinsi anavyohisi. Hii pia hupunguza shinikizo kwenye tumbo lake.

Mwanamume Ameketi

Mwanamume anaweza kuketi kwenye kiti au kitanda huku mwanamke akiwa juu yake.Katika staili hii, mwanamume anakuwa kwenye kiti au kitanda, ambayo inasaidia kuondoa uzito kutoka kwa tumbo la mwanamke.

Mwanamke Kulala Kando:

 

Mwanamke Kulala Kando:

Hii ni staili salama sana kwani inasaidia kupunguza shinikizo kwenye tumbo la mwanamke na inaruhusu urahisi katika kufanya tendo.

Je naruhusiwa kupiga punyeto badala ya tendo?

Fahamu kwamba daktari akishauri usifanye tendo anamanisha pia usifanye kitu chochote ambacho kinakuamsha hisia na kukufikisha kileleni mfano kutumia dildo an vidole

Hamu ya Tendo la Ndoa wakati wa Ujauzito

Kila mwanamke mwanamke mjamzito anatofautiana namna anavojisikia kuhusu tendo. Baadhi hamu ya tendo hupotea kabisa. Wengine hufurahia zaidi tendo na kupata msisimko zaidi wa mapenzi wakati huu.

Kipindi cha ujauzito ni kawaida kwa hamu ya tendo kubadilika. Muhimu zungumza na mpenzi wako namna unavojisikia. Mueleze unapenda staili ipi nzuri ya kufanya tendo isiyokuumiza.

Mambo ya Kuzingatia Wakati wa Kufanya Mapenzi

Ni muhimu kuzingatia mambo kadhaa ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto:

  1. Wasiliana na Daktari: Ni vyema kuzungumza na daktari kabla ya kuanza kufanya mapenzi ili kupata ushauri sahihi.
  2. Kusikiliza Mwili Wako: Ikiwa unahisi maumivu au discomfort yoyote, ni bora kusitisha shughuli hiyo.
  3. Kuepuka Staili Zenye Hatari: Staili ambazo zinahitaji mwanamke kulala tumboni zinapaswa kuepukwa kabisa.

Tendo la Ndoa Baada Ya Kujifungua

Kwa week 6 za mwanzo baada ya kujifungua inashauriwa usifanye tendo la ndoa. Sababu zikiwa unahitaji:-

  • kupona kidonda wendapo njia ya uke ilikatwa kidogo kuongeza mlango wa mtoto kutoka
  • kupona kidonda cha tumbo endapo kama ulijifungua kwa upasuaji
  • uchovu kutokana na kujifungua
  • mabadiliko ya homoni yatapelekea ukose hamu ya tendo kwa muda
  • baaada ya kuzaa ni kawaida kuendelea kupata bleed kwa week 4 mpaka 6
  • Stress kutokana na kuwaza sana kuhusu majukumu mapya kama mzazi

Kwa ujumla tendo la ndoa lifanyike baada ya mama kupona kabisa. Ongea na daktari wako akupe ushauri lini itakuwa sawa. Kwa kiasi kikubwa week 6 zinafaa kusubiri kabla ya kuanza tena tendo la ndoa. Muhimu hakikisha tu una utulivu kihisia na kimwili kabla ya kuanza .

MUHIMU:

Ni kweli katika kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujisikia kuchokachoka sana hali inayowafanya wasipende kushiriki tendo la ndoa, lakini hali huwa tofauti kwa wanaume wengi pindi wapenzi wao wawapo wajawazito kwani ni kipindi ambacho mwanaume hufurahia sana kushiriki tendo la ndoa na mjamzito kutokana na ukweli kuwa katika kipindi hiki mwanamke huwa na joto lakutosha sehemu zake za siri, joto ambalo humfanya mwanaume apagawe.
Hivyo mjamzito anapaswa kuhakikisha anafanya kila analoweza kumpa mwenza wake unyumba isipokuwa tu endapo atakuwa ameshauriwa na daktari kutoshiriki tendo la ndoa kwa sababu za kitaalam!..
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Burhoney
  • Website

Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika Ulimwengu wa Blogin ,Na Uandishi wa Makala Mbalimbali mitandaoni katika kuhakikisha nakuletea kilichobora nimekuwa nikitumia muda Wangu mwingi kujifunza juu ya mabadiliko ili kuendana na wakati

Related Posts

Aina Za Dawa Za Fangasi Ukeni

June 21, 2025

Dawa asili ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

June 21, 2025

Dawa Ya Kurekebisha Mzunguko Wa Hedhi

June 21, 2025
Leave A Reply Cancel Reply

SwahiliForums Ni jukwaa la Habari na Makala mbalimbaali kwa Lugha kiswahili Habari za Michezo,Elimu, Biashara,Ajira Mpya na Dondoo za Afya Endelea kutufuatilia kwa kutembelea site yetu SwahiliForums.com

Karibu kwenye Swahiliforums, jukwaa lako la kipekee kwa habari, maarifa, na mijadala inayoangazia masuala ya kijamii, uchumi, na utamaduni kutoka kwa mtazamo wa Kiswahili. Hii ni blog ambayo inalenga kutoa taarifa za kina kuhusu matukio ya sasa, maisha ya kila siku, na masuala muhimu yanayoathiri jamii zetu katika eneo la Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
© 2025 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.