Inawezekana ukawa Umeshika ujauzito lakini kutokana na Uchanga wa mita Baadhi ya vipimo vikashindwa kugundua au kusoma kama una mimba Ndio mana nimekuandalia makala hii iliyobeba dalili 30 za mimba changa ili ukiona dalili moja kati ya Hizi jua kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuwa una Ujauzito.
- Kutoona siku zako au Hedhi yako kwa Mjamzito.
- Kupata kichefu chefu na kutapika kwa Mjamzito.
- Kuchoka Sana Mara kwa Mara kwa Mjamzito.
- Kutokwa na Damu kama Matone kwa Mjamzito .
- Kulala Mara kwa Mara kwa Mjamzito
- Kutokwa na Ute mwingi Ukeni kwa Mjamzito.
- Matiti/Maziwa kuuma kwa Mjamzito.
- Kubadilika kwa Harufu kwa Mjamzito.
- Chuchu Kubadilika Rangi na kuwa nyeusi kwa Mjamzito.
- Matiti kuwa makubwa zaidi na kuongezeka Uzito kwa Mjamzito.
- Maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia kwa Mjamzito.
- Maumivu ya Kiunoni kwa Mjamzito.
- Maumuzi ya Mgongoni karibia na kiunoni kwa Mjamzito.
- Mapigo ya Moyo kwenda mbio ktk kipindi cha Ujauzito.
- Kujaa Mate Mdomoni mwa Mjamzito.
- Mdomo kuwa Mchungu kwa Mjamzito.
- Mjamzito kula Udongo.
- Tumbo la Mjamzito kujaa Gesi.
- Kupunguza hamu ya kufanya Tendo la Ndoa ktk kipindi cha Ujauzito.
- Kukojoa Mara kwa Mara katika kipindi cha Ujauzito.
- Kupata kiungulia ktk kipindi cha Ujauzito.
- Mjamzito kuwa na Chunusi Usoni.
- Mjamzito kuwa Mstari Tumboni ambao unatoka sehemu ya chini ya kifuani mpaka kwenye sehemu ya chini ya Kitovu karibia na mfupa wa Kinena.
- Tumbo la Mjamzito kuwa na Michirizi ktk kipindi cha Ujauzito.
- Mjamzito kutokwa na Damu Puani au kwenye Fizi/Meno katika kipindi fulani Cha Ujauzito.
- Baadhi ya Wajawazito hupata Bawasiri au vinyama vinavyokuwepo kwenye njia ya haja kubwa.
- Mjamzito Kupata maumivu ya Kichwa.
- Mjamzito kukosa Usingizi.
- Kubadilika kwa mhemuko au Mudi.
- Tumbo kuwa kubwa na kuongezeka katika kipindi cha Ujauzito Kutokana na ukuaji wa Mtoto Tumboni na nk.
Soma Hii : Je ni sawa kuendelea kunyonyesha mtoto wakati una mimba nyingine?
KUMBUKA; Dalili pekee hazitoshi kuonesha kuwa Mjamzito kuna Baadhi ya Magonjwa huwa na Dalili zinazofanana na Baadhi ya Dalili za Ujauzito,
Hivyo ni vema kuweza kufanya kipimo Cha Mimba Cha Mkojo (UPT) endapo unahisi kuwa na Ujauzito.
Kipimo hiki kinapofanyika siku ya 10 au 14 tokea Mimba kutungwa huweza kuonesha Majibu sahihi kwa asilimia 99% na endapo hakikuonesha Mimba na bado unapata Dalili za Mimba unaweza kurudia kipimo hiki siku 3 – 5 tokea ufanye kile kipimo Cha kwanza.