Halmashauri ya Wilaya ya Karatu imetoa tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa waombaji wa nafasi za kazi zilizotangazwa awali kupitia mfumo wa Ajira Portal. Tangazo hili limetolewa tarehe 12 Septemba 2025 na linaeleza ratiba, masharti na majina ya walioitwa kwenye usaili.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
- Usaili utafanyika kuanzia 15/09/2025 hadi 18/09/2025 kulingana na kada. 
- Kila msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho halali (Kitambulisho cha Mkazi, NIDA, kura, uraia, kazi au hati ya kusafiria). 
- Wasailiwa waje na vyeti halisi vya elimu na taaluma, kuanzia cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, Kidato cha VI, Astashahada na Stashahada kulingana na sifa za nafasi. 
- Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, na Result slips za Form IV & VI hazitakubalika. 
- Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi. 
- Waombaji waliomaliza nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na kuidhinishwa na TCU, NACTE au NECTA. 
- Kwa waombaji wa nafasi ya Udereva, lazima waonyeshe leseni halisi ya Daraja C au E pamoja na vyeti vya mafunzo. 
- Wasailiwa wote wanapaswa kunakili namba zao za mtihani kupitia akaunti zao za Ajira Portal kabla ya usaili, kwani hazitatolewa siku ya usaili. 
- Hali ya hewa ya Karatu kwa kipindi hiki ni baridi, hivyo wasailiwa wanashauriwa kuvaa nguo zinazostahimili ubaridi. 
- Waombaji ambao majina yao hayajaorodheshwa, watambue kuwa hawakukidhi vigezo, lakini wanahimizwa kuomba tena kwenye nafasi zijazo. 
Ratiba ya Usaili
Usaili wa Mchujo
- Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Karatu 
- Kada: Msaidizi Maendeleo ya Jamii Daraja la II 
- Tarehe: 17-09-2025 
- Muda: Saa 1:00 asubuhi 
- Mahali: Ukumbi wa Shule ya Sekondari Karatu 
Usaili wa Mahojiano
- Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Karatu 
- Kada: Msaidizi Maendeleo ya Jamii Daraja la II 
- Tarehe: 18-09-2025 
- Muda: Saa 1:10 asubuhi 
- Mahali: Ukumbi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu 
DOWNLOAD Majina ya Walioitwa kwenye Usaili
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

 


