Katika dunia ya kisasa, matumizi ya simu za mkononi yamekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku. Moja ya vipengele vinavyoleta mabadiliko katika utumiaji wa simu ni code za mitandao ya simu ambazo hutumika kutambulisha na kutofautisha mitandao mbalimbali ya simu. Katika makala hii, tutajadili orodha ya code za mitandao ya simu nchini Tanzania, pamoja na umuhimu wao kwa watumiaji wa huduma za simu.
Kwa mawasiliano ndani ya Tanzania namba za kieneo hutanguliwa na “0”. Kufikia simu kutoka nje ya nchi kuna namba ya kimataifa 00255 (sawa na +255) inayofuatiliwa na namba ya kieneo bila 0 na namba ya simu.
Aina ya itandao ya Simu Tanzania
Tanzania ni nchi endelevu katika swala la teknolojia kama yalivyokua mataifa mengine. Kwenye ulimwengu wa mawasiliano Tanzania pia imeshuhudia kukua kwake kwa kua na idadi kubwa ya makampuni yaa simu. Hapa chini ni kampuni za mawasiliano ya simu zinazopatikana Tanzania.
1. Tigo/Yasi
2. Vodacom
3. Airtel
4. Halotel
5. TTCL
6. Zantel
Namba za simu za mkononi
Namba hizi huanza kwa 6 au 7 na kuwa na tarakimu 9 (bila sifuri).
Simu za mkononi Tanzania | |
---|---|
Namba ya mtandao | Kampuni |
62 | Halotel (Viettel) |
65 | TIGO (Mobitel) |
66 | Smile Communications Tanzania Limited |
67 | TIGO (Mobitel) |
68 | Airtel Tanzania Limited |
69 | Airtel Tanzania Limited |
71 | TIGO (Mobitel) |
73 | TTCL Tanzania Telecommunications Company Ltd |
74 | Vodacom (Celtel) |
75 | Vodacom (Celtel) |
76 | Vodacom (Celtel) |
77 | Zantel (Zanzibar Telecom Ltd) |
78 | ZAIN |