Fangasi za Sehemu zasiri kama vile ukeni au kwenye Mapumbu kwa wanaume ni Ugonjwa unaowatesa Vijana wengi ,Tatizo au ugonjwa.Makala hii inakupa Muongozo sahihi wa kutibu fangasi kwa wanaume na wanawake.
Fangasi za ukeni ni nini?
DALILI ZA FANGASI UKENI
- Kuwashwa sehemu za siri.
- Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
- Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation).
- Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje/mashavu ya uke (labia minora).
- Kupata vidonda ukeni (soreness).
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi, mzito au majimaji.
- Kutoa harufu mbaya ukeni.
- Kuhisi kuungua sehemu za uke
- Kubadilika kwa rangi sehemu za siri
- Kuchubuka kwa ngozi au mipasuko ya uke
- maumivu wakati wa kukojoa haswa kwenye mashavu na uke, maumivu wakati wa kujamiiana.
Japo kuwa tatizo hili huwa si kubwa sana kwa wagonjwa wengi ila kuna baadhi ya wagonjwa huweza kupata changamoto hii kwa ukali zaidi kama sehem za siri kuwa nyekundu, kuvimba, na misitari katika kuta au mashavu ya sehem za siri.
Chanzo cha Fangasi za ukeni
Kama tulivyoeleza hapo awali, chanzo cha fangasi ukeni ni fangasi wajulikanao kitaalamu kama “candida albicans,” ambao kwa kawaida huishi mwilini. Tumesema pia katika baadhi ya watu, hawa kandida huweza kuongezeka na kusababisha maambukizi. Haya ni maambukizi ambayo huwapata sana wanawake na yanaweza kumkumba mwanamke wa umri wowote.
Mahali gani Fangasi (Candida Albicans) wanapokaa mwilini
Candida albicans hupatikana katika mdomo, mrija wa kupitishia chakula (koromeo), kibofu cha mkojo, uume au katika uke na kwenye ngozi pia, vilevile hupatikana kwenye tumbo, kwapa.
Bakteria hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta madhara, isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika mfano mabadiliko katika hali ya pH ambapo pH ya mwanamke ndani ya uke ni 4-4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine.
Hivyo pH hiyo inapovurugwa kutokana na magonjwa mbalimbali, pia kupungua kwa kinga ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali hupelekea kukua kwa Candida albicans, ndio maana wagonjwa wenye maradhi ya ukimwi na kansa, ama wanaopata matibabu ya mionzi huwa kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa na fangasi.
Maambukizi ya fangasi ukeni yanaweza isiwe ugonjwa hatari sana pale unapoanza lakini huleta usumbufu na harufu kali na hivyo mgonjwa kukosa raha na amani.
Kinga ya fangasi za ukeni
Wanawake wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua fangasi za sehemu za siri ukilinganisha na wanaume, lakini pia hata wanaume huambukizwa tatizo hili.
Kinga ni bora kuliko tiba. Ugonjwa huu unaweza kujikinga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kuzingatia kanuni ya afya na usafi. Kwa fangasi za ukeni zingatia haya:
- Osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa safi.
- Epuka mavazi yote ya kubana ukeni.
- Kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture mara kwa mara yatakusaidia kuepusha maambukizi ya fangasi ukeni.
- Epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys, diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni
- Epuka kutumia sabuni za kemikali/dawa kuoshea ukeni.
- Dumisha usafi sehemu za siri kwa maji safi.
- Epuka kuvaa nguo za ndani zisizoruhusu joto na unyevu kutoka.
- Punguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari.
WATU GANI WAPO HATARINI ZAIDI KUPATA TATIZO HILI
- Matumizi ya dawa za kuua vijidudu: Dawa hizi zinaweza kubadilisha usawa wa bakteria ukeni, na kusababisha ukuaji wa fangasi.
- Matumizi ya dawa za uzazi: Baadhi ya wanawake wanaweza kupata maambukizi ya fangasi kutokana na matumizi ya vidonge vya uzazi au vipandikizi.
- Mimba: Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito yanaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya fangasi.
- Ugonjwa wa kisukari: Wanawake wenye kisukari wanaweza kuwa na hatari kubwa ya maambukizi ya fangasi kutokana na viwango vya sukari kuwa juu.
- Matumizi ya dawa za steroid: Dawa hizi zinaweza kuathiri kinga ya mwili na kuongeza uwezekano wa maambukizi ya fangasi.
- Mabadiliko ya homoni: Mabadiliko katika viwango vya homoni vinaweza kusababisha maambukizi ya fangasi.
- Kuwasha au kusugua sana ukeni: Hii inaweza kusababisha usumbufu na kufanya fangasi kuota.
- Usafi mbaya wa maeneo ya siri: Usafi duni wa maeneo ya siri unaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya fangasi.
TIBA ZINAZOTUMIKA KUTIBU FANGASI UKENI
Matibabu ya maambukizi ya fangasi ukeni yanaweza kutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi na historia ya mgonjwa. Hata hivyo, chaguo la matibabu kwa kawaida hujumuisha:
1. Dawa za kupaka: Dawa za antifungal ambazo hupakwa moja kwa moja kwenye eneo lililoathirika, kama vile clotrimazole, miconazole, au terconazole. Dawa hizi zinapatikana kwa aina ya krimu, gel, au dawa za kuingiza ukeni (suppositories).
2. Dawa za kumeza: Dawa za antifungal zinazomezwa, kama vile fluconazole, zinaweza kutumika kwa maambukizi makali au yanayorudia mara kwa mara.
3. Tiba ya kimuuguzi: Matibabu haya yanaweza kujumuisha kubadilisha mitindo ya maisha kama vile kuvaa nguo zinazoruhusu hewa kupita, kuepuka kuosha ukeni kwa kutumia sabuni yenye harufu, na kudumisha usafi wa maeneo ya siri.
4. Ufuatiliaji wa hali: Ikiwa maambukizi yanaendelea au kurudia, daktari anaweza kupendekeza matibabu zaidi, kama vile kutumia dawa za kuua fangasi kwa muda mrefu zaidi au mara kwa mara.
5. Matibabu ya wenza: Katika baadhi ya visa, daktari anaweza kupendekeza matibabu kwa mwenza wa mgonjwa ikiwa maambukizi yamejitokeza mara kwa mara.
TIBA ZA ASILI AU TIBA LISHE KWA TATIZO HILI LA FUNGUS UKENI
Tiba hii ni kwa wale ambao wametumia njia nyingi na tofautitofauti kutibu fungus ila zote zimekataa yaani baada ya muda fungus zinarudi tena.
Kuna dawa maalum ya kuweza kuingozea ngozi yako uwezo wa kujikinga kutokana na maradhi yanayoshambulia ngozi yako.