Ugonjwa wa Pangusa (Trichomoniasis) ni mojawapo ya magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na vimelea vya protozoa vinavyojulikana kama Trichomonas vaginalis. Ingawa unaweza kuathiri wanaume na wanawake, mara nyingi huleta madhara makubwa zaidi kwa wanawake, lakini wanaume wanaweza kuwa waenezaaji wakuu wa ugonjwa bila wao kugundua.
Dalili za Ugonjwa wa Pangusa
Kwa wanawake:
Kutokwa na majimaji mengi ya ukeni yenye harufu mbaya
Majimaji hayo huwa ya rangi ya kijani, njano au kijivu
Kuwashwa kwenye uke na maeneo yanayozunguka
Maumivu wakati wa kujamiiana
Maumivu au hali ya kuchoma wakati wa kukojoa
Kuvimba kwa uke na midomo ya uke
Kuhisi joto au maumivu ya chini ya tumbo
Kwa wanaume:
Kutokwa na ute au majimaji kutoka kwenye uume
Maumivu wakati wa kukojoa
Kuwashwa kwenye mrija wa mkojo (urethra)
Hali ya kuchoma wakati wa kutoa mkojo
Kuwashwa sehemu ya kichwa cha uume
Wanaume wengi huwa hawana dalili kabisa
Sababu za Kuambukizwa Ugonjwa wa Pangusa
Ugonjwa wa pangusa husababishwa na uambukizaji wa vimelea vya Trichomonas vaginalis. Maambukizi haya hupitishwa kwa njia ya:
Kujamiiana bila kutumia kondomu na mtu aliyeambukizwa
Kugusana kwa karibu na sehemu za siri zenye maambukizi
Kutumia vifaa vya usafi wa mwili kama taulo au nguo ya ndani kwa pamoja
Mara chache sana, maambukizi yanaweza kupatikana kupitia vifaa vya kuogea au viti vya choo vya pamoja
Madhara ya Pangusa Iwapo Haitatibiwa
Maambukizi ya muda mrefu kwenye njia ya mkojo
Kuongezeka kwa hatari ya kupata au kusambaza virusi vya HIV
Maambukizi ya mara kwa mara kwenye uke au uume
Kwa wanawake wajawazito, inaweza kusababisha kujifungua kabla ya wakati au mtoto kuzaliwa na uzito mdogo
Msongo wa mawazo na matatizo ya kisaikolojia kutokana na kutokua na amani ya ndoa au uhusiano
Dawa za Kutibu Ugonjwa wa Pangusa
Ugonjwa huu unatibika kwa kutumia dawa za antibiotic zifuatazo:
1. Metronidazole (Flagyl)
Dawa ya kwanza kupendekezwa na madaktari
Hupatikana kwa dozi moja au kwa siku 5 hadi 7
Ni muhimu kuepuka pombe wakati wa kutumia dawa hii
2. Tinidazole
Hufanya kazi kama Metronidazole lakini inaweza kuwa na madhara machache zaidi
Hupendekezwa kwa watu wanaopata mzio kutokana na metronidazole
Vidokezo Muhimu Katika Matibabu
Hakikisha unamaliza dozi yote ya dawa kama ulivyoelekezwa
Wote wawili kwenye uhusiano wanapaswa kutibiwa kwa wakati mmoja
Epuka ngono hadi utakapo maliza tiba na uthibitishwe umepona
Usitumie dawa za kienyeji bila ushauri wa daktari
Njia za Kujikinga na Maambukizi ya Pangusa
Tumia kondomu kila unapojamiiana
Epuka kuwa na wapenzi wengi wa kingono
Fanya vipimo vya afya ya uzazi mara kwa mara, hata kama huna dalili
Zingatia usafi binafsi wa sehemu za siri
Wasiliana na mwenza wako kuhusu afya ya uzazi na vipimo vya magonjwa ya zinaa
MASWALI YAULIZWAYO MARA KWA MARA (FAQs)
Je, Pangusa ni ugonjwa hatari?
Ugonjwa huu si hatari sana ikiwa utatibiwa mapema, lakini unaweza kuleta madhara makubwa ikiwa hautatibiwa, ikiwemo kuathiri mfumo wa uzazi.
Naweza kupona bila kutumia dawa?
Hapana. Pangusa haitapona yenyewe bila tiba ya antibiotic. Dawa kama metronidazole au tinidazole ni muhimu.
Ni muda gani dalili huanza kuonekana baada ya kuambukizwa?
Dalili zinaweza kuanza kati ya siku 5 hadi 28 baada ya maambukizi, lakini wengine hawaonyeshi dalili kabisa.
Nifanye nini nikigundua mwenza wangu ana pangusa?
Unapaswa kwenda kupimwa na kuanza tiba haraka hata kama huna dalili. Pia jiepushe na tendo la ndoa hadi wote mponwe.
Je, kuna dawa ya asili ya kutibu pangusa?
Hakuna ushahidi wa kitaalamu unaothibitisha dawa za asili kutibu pangusa kikamilifu. Tiba salama ni kutumia dawa za antibiotic zilizoidhinishwa na daktari.